DIWANI
wa Kata ya Mtibwa wilayani Mvomero wa Chama cha CHADEMA, Luka
Mwakambaya, ametangaza vita na Mwenyekiti wa Chama Tawala (CCM), Seif
Sekilojo, Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Mohamedi Kidevu, na Mtendaji wa
Mji Mdogo wa Madizini, Saimon Muyogo, kwa kutengeneza mazingira ya
Kulamba asilimia 20% ya fedha za MKUKUTA.
Mwakambaya
alitangaza vita hiyo hadharani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
J’mosi Agosti 10, mwaka huu, huku Mwenyekiti wa CUF Kindevu, akiwepo
uwanajani hapo hapo akimuona na kumsimsikiliza .
Vita
ya Mwakambaya na Viongozi hao, inatokana na kuwapotosha wananchi wa Mji
huo kuhusu Maagizo ya Baraza la Madiwani ya Halmashauri ya Mvomero
kwenye Kabrasha, kuhusu matumiza ya fedha za MKUKUTA zaidi ya Mil. 32/-
zilizoamuliwa zitumike kumalizia miradi inayosuasua.
“Mimi
ndiye Rais wa Kata ya Mtibwa. Nimegundua Paka akitoka Panya anatawala,
hivyo sitakubali wakati huu wa Njaa Kali, wananchi wadanganywe na
kuchangishwa Michango ya Miradi inayosuasua, wakati Madiwani
tulishafanya maamuzi ya matumizi ya fedha hizo”.alisema Mwakambaya
Aliongeza,
“Sipo tayari kuona wananchi wanachangishwa fedha zinazoitwa za
maendeleo, kumbe mnawafanya wawalishe na kuwasomeshea watoto wenu!
Nasema fedha hiyo ndiyo itakayotumika..Nilikataza wasilipe Ushuru na
Michango na Mkuu wa Wilaya anajua hilo”.
Mwakambaya
aliwafumbua macho wananchi kuwa, Serikali ya CCM Mji Mdogo wa Madizini
inadaiwa zaidi ya Mil. 3/-, Kunke zaidi ya Mil.1/- na Kidudwe zaidi ya
Mil.1/-, wakidai wamekopa Vifaa vya Ujenzi kwa matajiri wanataka walipe.
“Wananchi
kataeni; watajua watakakopata fedha hiyo, wanataka kuwafanya Punda ili
mchange muwalishie na kuwasomeshea watoto wao, na mimi sikubali fedha ya
MKUKUTA iende huko, Patachimbika!” alishangiliwa Mwakambaya.
Aidha
Mapema kwenye kikao cha Baraza Maendeleo la Kata (BMK), Wenyeviti wa
Vijiji walikubaliana na kuridhia matumizi ya Fedha hiyo akiwemo
Sekilojo, lakini huyo huyo alikataa akidai CCM kimemwagiza akatae, na
Kidevu akidai watakwenda Mahakamani, Mwakambaya akidai wanataka mwanya
wa kuzifuja fedha hizo.
Post a Comment