Mwenyekiti wa Yanga na kamati yake ya Utendaji wameibuka kidedea kwa upande wao kuwa na nguvu zaidi
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Taarifa
zilizotufikia katika dawati la michezo la Mtandao huu kutoka chanzo
chetu muhimu zinasema hatimaye Mkutani ulioitishwa na Wizara ya habari,
vijana, utamaduni na mchezo chini ya waziri wake, Mhe. Dkt. Fenella
Mukangara kuliweka sawa suala la mgogoro wa mkataba wa mauzo ya haki za matangazo ya Television kwa ligi kuu soka Tanzania bara uliowashirikisha
kamati ya ligi kuu ya TFF, klabu ya Yanga na Azam Media umemalizika
hivi punde huku maamuzi kadhaa yakifikiwa baina ya pande zote.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, mkutano huo umeamuru kuwa baadhi vipengele vya
mkataba huo kupitiwa upya kwa umakini kati ya kamati ya ligi na klabu ya
Yanga, na vile ambavyo vitakuwa tofauti virekebishwe kabla ya kuanza
kwa mchakato mzima wa kuwapa raha wanamichezo nchini Tanzania kutokana
na kuoneshwa kwa mechi hizo.
Pia
makubaliano yamefikiwa kuwa Uongozi wa Yanga utakaa kikao na Azam Media
kuzungumzia mambo mbalimbali ambayo Yanga imeonekana kuwa na shaka nayo
kuhusu Azam Media.
Mtandao
huu unafanya jitihada za kupata taarifa zaidi kuhusiana na Mkutano huo
muhimu sana kwa hatima ya soka la Tanzania, endelea kufuatilia kupitia
mtandao huu uliosheheni habari za moto moto.
Kati
ya klabu 14 za ligi kuu soka Tanzania bara, Yanga pekee ndio klabu
iliyokataa mkataba wa Azam Media kwa kutoa sababu mbalibali, na
Mwenyekiti wake Yusuf Manji kuitisha mkutano wa dhararu wa wanachama
utakaofanyika Agosti 18 kujadili suala hilo.
Post a Comment