![]() |
| Seif Shabaan Mohamed |
KATIBU
Mkuu mpya wa Jumuia ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Seif Shabaan
Mohamed ameonya kuwa hatakuwa na huruma na kiongozi yeyote atakayefuja
fedha za jumuia hiyo.
Alisema katika kipindi cha miaka mitano cha uongozi wake atahakikisha anafanyakazi kwa uadilifu na uamini mkubwa na kwamba atakuwa mkali na makini kuhusu matumizi ya fedha za jumuia yake.
Alisema katika kipindi cha miaka mitano cha uongozi wake atahakikisha anafanyakazi kwa uadilifu na uamini mkubwa na kwamba atakuwa mkali na makini kuhusu matumizi ya fedha za jumuia yake.
Mohamed
alisema kila kiongozi anastahili kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu,
maadili na miiko kwa kutokana na dhamana aliyonayo na si vinginevyo.
Kauli Katibu Mkuu
huyo mpya imekuja huku jumuia hiyo ikiwa imegumbikwa na wingu jeusi la
matumizi mabaya ya fedha na hivyo kuifanya isue sue kwa kipindi kirefu
badala ya kusonga mbele.
Aliyasema hayo jana
katika ukumbi wa Dodoma Hoteli wakati akiwashukuru Wajumbe wa Baraza Kuu
la Jumuia ya Wazazi kwa kumthibitisha kushika wadhifa huo.
Mohamed anashika
nafasi hiyo kwa mara ya kwanza baada ya aliyekuwa akiishikilia Khamis
Suleiman Dadi kutoteuliwa tena na vikao vya juu vya CCM.
“Kwanza nashukuru
kupata nafasi hii ya juu maana sikutegemea kama ingekuwa hivi, lakini
niwaambie kwamba nitakuwa mkali sana na masuala fedha,” alisema Mohamed.
Hata hivyo,
aliwataka viongozi wenzake wampe ushirikiano wa kutosha ili kifikisha
malengo ya jumuia hiyo kuwa katika hali nzuri zaidi.
“Binafsi nitafanya kazi kwa karibu sana nikishirikiana na na nyinyi wenzangu hivyo, nanyi mnipe ushirikiano,” alisema.
Mbali na Katibu Mkuu
huyo mpya, jumuia hiyo imefanya mabadiliko makubwa ya kiongozi baada ya
kupata Manaibu Makatibu Wakuu wapya.
Manaibu hao ni Glorious Luoga (Bara) na Najma Murtaza Giga (Zanzibar).
Akizungumza na
viongozi hao, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallahman
Kinana aliwapongeza viongozi hao kwa kushika wadhifa huo na kuwataka
wafanye kazi kwa uadilifu na kwa kasi kubwa.
“Kwanza nimpongeze mwenyekiti wenu Bulembo na viongozi wenzake kwa kuifanya jumuia hii sasa isikike kila kona.
“Jumuia hii ilikuwa
inakufa, lakini sasa kila unakopita unasikia Bulembo kapita na anafanya
mambo makubwa sana ya kuipigania jumuia na Chama chake,” alisema Kinana.
Hata hivyo Kinana alimtaka Bulembo na viongozi wenzake kuongeza kasi ya kuiimarisha jumuia hiyo ili iwe na nguvu zaidi.
Kwa upande wake
Bulembo alisema amejipanga kikamilifu kwa kuishirikiana na viongozi
wenzake ili kuidishia hadhi yake jumuia hiyo.
“Sisi tumejipanga
kikamilifu…tutakimbia huku na kule kwa ajili ya kukisemea chama chetu
kwa mazuri iliyoyafanya huku tukifufua uhai wa jumuia yetu,” alisema.
Bulembo aliutaka uongozi mpya wa sasa wa jumuia hiyo kukaa kama timu moja na kuchapakazi kwa ushirikiano wa karibu.



Post a Comment