|
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid na Balozi wa Italia
nchini Pierluigi Velardi wakizindua maabara ya kisasa kwenye majengo ya
Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) huko Bagamoyo hivi karibuni. Maabara
hiyo ambayo ina uwezo wa kutambua magonjwa mapya na yale ya hatari
sana ikiwemo Ebola bila kuhatarisha maisha ya watafiti inajulikana
kitaalamu kama Biosafety Lab 3, na ni ya kwanza ya aina yake katika
eneo la Afrika Mashariki na Kati. Maabara hiyo yenye thamani ya
Shilingi bilioni 1.2 imejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Italia na
inasimamiwa na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) | | | |
|
|
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr Seif Rashid hivi karibuni
amezindua maabara ya kisasa kabisa ambayo ina uwezo wa kutambua magonjwa
mapya na yale ya hatari sana ikiwemo Ebola bila kuhatarisha maisha ya
watafiti inayojulikana kitaalamu kama Biosafety Lab 3 ambayo ni ya
kwanza ya aina yake katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Maabara
hiyo yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.2 imejengwa kwa ufadhili wa
Serikali ya Italia na inasimamiwa na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI)
kwenye maabara zake za Bagamoyo. Pichani anaonekana Mratibu wa mradi wa
maabara hiyo Bw.Francesco Vairo akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa
Afyya (wa pili kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (
WHO) Dr. Rufaro Chatora na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi
wakiwa ndani ya maabara hiyo. |
on Friday, August 2, 2013
Post a Comment