Katika Operesheni ya Kuzuia Uhalifu na Madawa ya Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha liliingia kijijini hapo majira ya saa 2 za asubuhi Agosti 13 mwaka huu.
Ilikuwa ni ziara ya
kushtukiza katika kijiji hicho hali iliyowafanya wanakijiji kutaharuki na kuanza
kukimbia na kutokomea milima wakiziacha nyumba zao zikiwa
wazi.
Uongozi wa Kijiji
hicho nao ulitoweka kusikojulikana kwa kuhofia mkono wa Jeshi la
Polisi.
Kamishna wa Operesheni
hiyo ACP Ngonyani alisema safari hii waliamua kwenda baada ya mavuno kutokana na
ukweli kwamba zikiwa bado shamabni ni kazi nzito sana ya
kufyeka.
ACP Ngonyani aliongeza
kusema magunia 225 ya zao hilo haramu nchini Tanzania waliamua kuyateketeza
kutokana na namna ya kuyasafirisha kuwa mgumu.
Mkuu wa Operesheni
hiyo alisema operesheni hiyo bado ni endelevu katika kijiji hicho kwa mwaka huu
ni mara ya pili lakini wamegundua mbinu mpya.
Pia alisema magunia
127 na watuhumiwa watano wamewasafirisha hadi makao makuu kwa hatua zaidi za
kisheria.
Wanakijiji
wameilalamikia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jeshi la Polisi
kuwa zao hil ni muhimu kwa familia zao kwani wanapoliuza husomeshea watoto wao
na mahitaji mengine ya kifamilia.
JAIZMELALEO katika operesheni
hiyo ilishuhudia nyumba moja ya kijana wa kidato cha Nne ikiwa na
magunia mawili ya Bangi na baada ya uchunguzi zaidi mwanafunzi huyo alidai kuwa
alivuna ili auze akalipe ada na mahitaji mengine ya
kifamilia.
Imebainika kwamba guni
moja linapouzwa kutoka shambani hutoa kiasi cha zaidi ya shilingi 100,000/= za
Tanzania.
Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amewataja watuhumiwa waliokamatwa katika
operesheni hiyo ambayo imevunja rekodi ya zilizopita kuwa ni Nemali Saitoti
(50), Esuba Daudi (33), Thomas Lesnoi (63), Lomayan Thomas (27) na Natumi Daudi
(29).
ACP Sabas amesema
opersheni hiyo ni endelevu na amewataka wananchi, wakulima na watumiaji kuacha
kuendeleza zao hilo kwani ni kinyume cha sheria huku akiwataka kuendeleza Polisi
Jamii na Ulinzi Shirikishi.
Post a Comment