Mgambo wa Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa na viongozi mbali mbali wakielekea kuvunja nyumba zilizojengwa
makaburi ya Mtwivila leo
Mgambo wa Manispaa ya Iringa na
mwanasheria katikati Bw Innocent Kihaga wakielekea kuvunja nyumba
zilizojengwa makaburini Mtwivila
Mgambo wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakivunja nyumba iliyojengwa katikati ya makaburi ya Mtwivila
Kaburi hili la Rashid M. Lukuvi likiwa jirani kabisa na ukuta wa nyumba hiyo iliyovunjwa
Mgambo wakivunja nyumba iliyokuwa ikijengwa katika makaburi ya Mtwivila mjini Iringa leo
Nyumba iliyojengwa makaburini yavunjwa rasmi leo na mgambo wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Makaburi yaliyozunguka nyumba hiyo
Hii ndio nyumba ambayo ipo jirani na
kaburi la marehemu Idd Chonanga aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli
kaburi lenye mashada kushoto ,na hapo waliposimama mgambo ndipo
alipokaa waziri mkuu Mizengo Pinda wakati wa mazishi na viongozi mbali
mbali wa mkoa wa Iringa
Uvunjaji wa nyumba ambayo nje katika
msalaba hapo ndipo waziri mkuu Mizengo Pinda alikaa wakati wa mazishi
ya diwani Chonanga ,nyumba hii imevunjwa sehemu ya ukuta na mmiliki
wake amepewa siku 30 kuanzia leo kuivunja
Mgambo wakivunja nyumba iliyojengwa eneo la makaburi ya Mtwivila mjini Iringa
Wananchi ambao wamezika ndugu zao katika makaburi hayo wakishuhudia zoezi hilo
HATIMAYE
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeivunja nyumba iliyokuwa
ikijengwa katikati ya makaburi ya Mtwivila ambayo iliripotiwa na
mtandao huu na vyombo mbali mbali vya habari likiwemo gazeti la
Jamboleo , radio Ebony Fm na radio Cloud FM pamoja na nyumba
nyingine mbili ambazo pia zilikuwa
zikianzwa kujengwa eneo hilo .
Pamoja na kuendesha zoezi la
kuzivunjwa nyumba hizo ambazo zilikuwa katika hatua ya mwanzo
kabisa pia Halmashauri hiyo imetoa muda wa siku 30 kuanzia leo
kwa mmiliki wa nyumba nyingine iliyokutwa imekamilika ambayo pia
imejengwa karibu na makaburi ya Mtwivila eneo ambalo waziri Mkuu Mizengo
Pinda alikaa wakati wa mazishi ya aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli
marehemu Iddi Chonanga
Hatua ya kuvunjwa kwa makaburi hayo
imekuja ikiwa ni siku mbili zimepita baada ya mtandao huu wa matukio daima kuibua suala hilo kuibua
ujenzi huo holela na ni siku moja baada ya mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya Manispaa Bi Terresia Mahongo kutoa agizo kwa maofisa
mipango miji , afisa ardhi na mwanasheria wa Manispaa ya Iringa
kufika eneo hilo ili kuchukua hatua sitahiki.
Zoezi la
kuvunja nyumba hizo leo majira ya saa 3 asubuhi limeongozwa na
maofisa mbali mbali wa Manispaa ya Iringa akiwemo mwanasheria wa
Halmashauri hiyo Bw Innocent Kihaga pamoja na mgambo zaidi ya watano
wa Halmashauri hiyo.
Kuvunjwa kwa nyumba hizo kumeshuhudiwa
na umati mkubwa wa wananchi wa maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa
ambao walifika kushuhudia utekelezaji wa agizo la mkurugenzi baada
ya baadhi yao kudai wamiliki wa nyumba hizo wamejenga katika
makaburi ya ndugu zao hivyo walikuwa wakishindwa kuchukua hatua
kutokana na kutojua wahusika wa ujenzi huo wa nyumba makaburini.
Miongoni
mwa makaburi yaliyokuwa hatarini kuvunjwa na wajenzi wa nyumba hizo
ni pamoja na kaburi la Rashind M. Lukuvi ambalo lilikuwa hatarini
kuvamimiwa na wajenzi hao iwapo ujenzi huo ungefumbiwa macho.
Wakipongeza
hatua iliyochukuliwa na uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa wananchi waliofika eneo hilo kushuhudia zoezi akiwemo
Yustina Malinga , Yohana Sanga na Juma Ally walisema kuwa mbali
ya kupongeza uongozi wa Manispaa chini ya mkurugenzi wake Bi
Mahongo kwa kuchukua hatua ila bado waliwataka wananchi wenzao
wanaoendelea kujenga makaburini kuwa na huruma na marehemu
waliozikwa katika maeneo hayo kwani watambue kuwa hata hao marehemu
walikuwa kama wao .
Alisema Bi Malinga kuwa wakati
mwingine wananchi wamekuwa wakiitafua ugomvi serikali kwani
kitendo cha kujenga katika makaburi ni kinyume na tamaduni za
kitanzania na kuwa makaburini ni eneo la kuishi wafu sasa mtu
mzima na familia yako kujenga makaburini utajiweka katika mazingira
ya kuogopwa na kila mtu.
Huku kwa upande wake mzee Sanga
akisema kuwa mbali ya wananchi hao awali kuonekana wakilima maeneo
hayo ila bado baada ya kuona hakuna mtu anayewafuatilia waliamua
kujenga kabisa.
"Tunawaomba hawa ndugu ambao inasemekana si wenyeji wa eneo kutumia utu kabla ya kuanza kuvamia makaburi yetu na kuanza kujenga nyumba juu ya makaburi ya ndugu zetu.....pia tunaomba wahusika wasakwe ili wachukuliwe hatua kali za kisheria"
Mbali ya kutaka wahusika hao kusakwa bado walielekeza lawama zao kwa watendaji wa mitaa na kata kwa kushindwa kuwawajibisha wananchi wanaojenga kiholela katika milima na maeneo ya makaburi kama hayo.
Mwanasheria wa Manispaa ya Iringa Bw Kihaga alisema kuwa wamelazimika kuvunja nyumba hizo baada ya kuonekana zimejengwa maeneo ambayo si rasmi na bila kibali cha mipango miji .
Hata hivyo mwanasheria huyo alisema wametoa muda wa siku 30 kwa mmiliki wa nyumba iliyopo jirani na makaburi eneo ambalo waziri mkuu Mizengo Pinda alikaa wakati wa mazishi ya diwani Chonanga kuivunja nyumba hiyo ndani ya siku 30 kuanzia leo kabla ya kuvunjiwa nyumba hiyo na kufikishwa mahakamani.
Pia alisema kuanzia sasa msako mkali kwa wote waliojenga maeneo ambayo si rasmi na wale wanaojenga bila vibali litaanza katika mji mzima wa Iringa na kuwataka wananchi wanaotaka kujenga kufuata sheria ya ujenzi ikiwa ni pamoja na kutafuta ardhi halali na kabla ya kujenga ramani zao kupitisha ili kupewa kibali cha ujenzi zaidi ya hapo watachukua hatu.
Awali mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bi Mahongo aliwataka wananchi kuheshimu sheria na kuwa hatakubali kuona ujenzi holela unaendelea katika maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kufichua watu wanaojenga nyumba kiholela na kuvamia maeneo ya wazi .
Hata hivyo kutokana na uchunguzi wa kina uliofanywa na mtandao huu wa www.matukiodaima.com umebaini kuwepo maeneo mengi zaidi ambayo wananchi wamejenga kiholela yakiwemo maeneo ya Mtwivila ,Mwang'ingo , Zizi la Ng'ombe, Ipogolo na Semtema ambako wananchi wameamua kujenga hadi katika vilele vya milima .
Post a Comment