Kirstie Trup (18) kabla ya kumwagiwa tindikali.
MMOJA wa wasichana waliomwagiwa tindikali Visiwani Zanzibar, Kirstie Trup, ameruhusiwa kutoka hospitalini.
Hospitali ya Chelsea and Westminster wanapotibiwa wasichana hao.
Kirstie Trup (18), aliyemwagiwa tindikali akiwa na mwenzake Katie Gee (18) wiki iliyopita ameruhusiwa mwishoni mwa wikiendi kurudi nyumbani kwao Hampstead, jijini London mpaka Alhamisi ya wiki hii ambapo atarudishwa katika hospitali ya Chelsea and Westminster kwa matibabu zaidi. Wakati mwenzake akiruhisiwa, Katie yeye bado anaendelea kupata matibabu katika majeraha yake ambapo aliungua kwa asilimia 80 ya mkono wake wa kulia na asilimia 50 ya sehemu za kifua na tumboni.Chanzo Global Publishers Blog

Post a Comment