Na Mwandishi Wetu, Dar
KATIKA
Kuelekea Redds Miss Ilala Ijumaa, leo kutakuwa na shindano la kumtafuta
mrembo mwenye kipaji (Talent) itakayofanyika katika mgahawa wa City
Sports and Loungeu liopo katikati ya jiji.
Mratibu wa
shindano hilo, Juma Mabakila alisema kuwa maandalizi ya kuelekea
shindano hilo yanaendelea vizuri na kueleza kuwa warembo wote 14
wamejipanga kuonesha vipaji vyao ipasavyo.
Mabakila
alisema mshindi wa talent atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya
shindano hilo ambalo litafanyika Ijumaa ijayo katika ukumbi wa Golden
Jubilee Tower ulipo katikati ya jiji.
Mratibu
huyo wa Ilala alisema mbali ya burudani hiyo, pia watatumia nafasi hiyo
kuuza ticket za VIP ambazo ni chache kwa watu maalum, lakini kutakuwa
na bahati nasibu itakayotoa pasi za bure za kusingia katika onesho la
Ijumaa.
Alisema
kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa
wilaya ya Ilala maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo
mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.
“Tumejipanga
vizuri kuonesha shoo nzuri kuanzia hii ya telent na ile kubwa Ijumaa,
kutakuwa na vitu tofauti na ilivyokuwa mwaka jana, kweli mambo
yanakwenda vizuri,” alisema Mabakila.
Mashindano
ya Redd's Miss Ilala yamedhaminiwa na Redd's Original,magazeti ya Jambo
Leo, Tanzania Daima,Smile, CXC Safaris, Blog ya wananchi, Fredito na
Dodoma wine
Post a Comment