Habari
zilizotufikia punde toka Bukoba zinasema Chama cha Mapinduzi-CCM Mkoani
Kagera kimewafukuza madiwani wanane wa chama hicho na kuwavua nyadhifa
zote walizokuwa nazo. --- (ITV)
-------------
Katibu wa CCM mkoa amemaliza press conference hi vi punde na kufafanua kuwa Halmashauri Kuu ya Mkoa imemaliza kikao chake hivi punde na kuamua madiwani nane wa manispaa ya Bukoba kufukuzwa katika chama na kufutwa nyadhifa zao za udiwani kutoka na mgogoro uliokuwa ukiendelea.
Majina ya madiwani hao nane waliofukuzwa ni haya yafuatayo:-

- Richard Gaspar (Miembeni )
- Murungi Kichwabuta (Viti maalum)
- Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)
- Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)
- Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)
- Robert Katunzi (Hamugembe)
- Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na
- Dauda Kalumuna (Ijuganyondo)
------------
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera Avelin Mushi, imesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa kutokana na chama kujali maslahi ya wananchi tofauti ya watu binafsi.
Mushi amesema kuwa kufukuzwa kwa madiwani hao ni kutokana na mgogoro ulidumu kwa muda mrefu juu ya Mbunge na Meya ambapo Rais Kikwete akiwa ziarani Kagera alitoa agizo la wanachama hao kutoendelea na mgogoro huo lakini maagizo hayo yalipuuzwa.
Pia, amesema kuwa vikao vya chama vimekuwa vikiendelea kwa kufuata kanuni na taratibu kwa kuwaonya juu ya kuhujumu serikali ya CCM kwa kushirikiana na madiwani kambi ya upinzani kutotekeleza maendeleo ya wananchi lakini wahusika wote wamekuwa wakikahidi maagizo ya kuitwa kwenye vikao. (CCM Chama blog)
Post a Comment