Hii ndiyo hati ya Ushindi tuliyopewa na TASO
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus
Kinawilo aliye simama Mbele akipokea Maelezo ya Kina juu ya Mbeya yetu
Blog inavyofanya kazi na mitandao mbalimbali ya Kijamii kutoka kwa
Mtaalam wa Mambo ya Mitandao ya Digitali kutoka Tone Multimedia Group
Fredy Anthony, alipo tembelea katika Banda la Mbeya Yetu Blog.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa Mh. Dr. Christine Ishengoma aliyevaa kofia akipokea
Ufafanuzi wa Jambo Kuhusu Blog ya Mbeya yetu kutoka kwa Msimamizi Mkuu
wa Mtandao wa Mbeya yetu Ambaye Pia ni mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni
ya Tone Multimedia Ndugu Joseph Mwaisango wa Pili kutoka Kushoto
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma akitaka kupata ufafanuzi wa
jinsi gani Mbeya yetu Blog tunavyopata habari na kuziweka kwa Muda kama
alivyo kuta tukio lake likiwa Live mara alipotembelea Banda la Mbeya
yetu na kujionea mwenyewe.
Kutoka
Kushoto ni Venance Matinya na David Nyembe wote kikosi kazi cha Mbeya
yetu Blog, wakiwa wanapita Mbele kuonesha Bango la Mbeya yetu kwa Mgeni
Rasmi wakati wa sherehe za Kilele cha siku ya Wakulima Nane nane Mbeya.
Msimamizi
Mkuu wa Mtandao wa Mbeya yetu Ambaye Pia ni mmoja wa Wakurugenzi wa
Kampuni ya Tone Multimedia Ndugu Joseph Mwaisango akipokea Hati ya
Ushindi kutoka kwa Mgeni Rasmi aliyevaa Skafu Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya Mh. Capt (RTD) Aseri Msangi
Baadhi
ya kikosi kazi cha Mbeya Yetu Blog, Kutoka kushoto ni Venance Matinya,
Joseph Mwaisango, Ezekiel Kamanga na Fredy Anthony.
MBEYA, Tanzania
Chama Cha Wakulima Tanzania (TASO) kanda ya Nyanda za juu Kusini, kimeutunuku cheti mtandao wa kijamii wa www.mbeyayetu.blogspot.com ambao upo chini ya Tone Multimedia Company Limited kutokana
na kuibuka mshindi wa kwanza wa kurusha matangazo kwa njia ya
Kidigitali katika maonesho ya Wakulima nanenane yaliyofanyika katika
viwanja vya John Mwakagale Uyole Jijini Mbeya.
Tuzo
hiyo imekuja kutokana na kikosi cha Mtandao huu kuweka kambi katika
maonesho hayo na kufanya shughuli za kurusha matangazo moja kwa moja
kutoka uwanjani hapo na kuwapagawisha wakulima ambao walipata fursa ya
kutembelea banda letu na kujionea habari zilizotokea muda huo huo na
kuonekjana hewani.
Mbali
na wakulima na watu mbali mbali waliokuwepo uwanjani hapo pia viongozi
wa Taso na wakuu wa Mikoa pia walipata fursa ya kutembelea banda la
Mtandao huu katika ziara zao za kukagua mabanda na hivyo kutoa sifa kwa
wamiliki wa Mtandao huu namna habari zilivyokuwa zikienda kwa wakati.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus
Kinawilo ndiye aliyekuwa wa Kwanza kufanya ziara hiyo na kukuta habari
zake tokea akipokelea mlangoni hadi kufikia mabanda habari zilikuwa
hewani, mwingine alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk. Christine
Ishengoma ambaye pia alionekana kuufagilia mtandao huu kwa namna
walivyoweza kutangaza Nanenane iliyofanyika kikanda na kuonekana kama
ni Kitaifa.
Aidha
kufuatia mchango huo wa Taso na wakulima kwa ujumla Uongozi wa Tone
Multimedia Group Kupitia Mbeya Yetu Blog unatoa shukrani kwa wote
waliuofanikisha shughuli za Nanenane hadi zinafikia kilele Agosti 8, na
kupelekea kupata cheti cha ushindi.
Tunapenda
kuwashukuru TASO kwa namna ya pekee, SBC (T) Ltdkupitia kinywaji chao
cha Pepsi, Shirika la Bima ya Afya (NHIF) kwa kutupatia gazebo
lililotusitili tukiwa kazini na wengine wengi ambao hatutaweza kuwataja
majina lakini tunaahidi kuendelea kushirikiana kwa pamoja.
Pia
tunapenda kuwashukuru Bloggers wote na waandishi wa habari kwa ujumla
hatutaweza kutaja kila chombo lakini tumekuwa pamoja mpaka kufanikisha
yote haya.
Mwisho
kabisa Tunapenda kukushukuru wewe Mdau wetu Mkubwa wa Mbeya yetu Blog
kwa kuonesha Moyo na Kutembelea kila wakati mtandao huu, Tunasema
asanteni sana, Bila nyie sisi hatuwezi fanya kazi.
Post a Comment