Mwenyekiti
wa Muungano wa Wanajeshi wastaafu Tanzania (MUWAWATA),Assedy Rajabu
Mayungi(kilia)akitoa tamko mbele ya waandhi wa habari (hawapo pichani)
jana kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es
salaam,kuzuia mikutano isiyo halali ya watu wanaopotosha
MUWAWATA(katikati)Mjumbe,Lenson Tupate(kulia)Mjumbe.Chalesi Sabugo.
Na Philemoni Solomon wa fullshangwe
“Ninatamka
kwamba kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi mkuu wa MUWAWATA TAIFA
uliofanyika tarehe 20/10/2013 mjini Dodoma ambao ndio ulioniweka
madarakani bado ninaendelea kuwa Mwenyekiti wa MUWAWATA TAIFA mpaka pale
kipindi changu cha miaka mitano kukaa madarakani kitakapomaliziaka kwa
mujibu wa sheria na si vingenevyo,na hii inatokana na katiba ya MUWAWATA
kwa mujibu wa cheti cha usajili Namba S.A.17184 ACT.CAP 337 C.R.E.2002
kilichotolewa tarehe 27/12/2012 na msajili wa vyama hiari toka Wizara ya
Mambo ya ndani ya nchi”alisema Mayungi,
Aliendelea
kusema,kuanzia tarehe ya leo mikutano yote ya Taifa,Mikoa,Wilaya na
kata inayofanywa na kikundi haramu kinachojiita kamati ya MUWAWATA
mapito ambayo haipo kikatiba isifanyike,wanachama wa MUWAWATA
mnapotoshwa na kundi hilo,kikao chochote kitakachofanyika baada ya tamko
hili ni batili na hatua kali za kisheria zitachukuliwa mara moja,fomu
zilizoandaliwa na kikundi hicho pamoja na kadi ni batili msikubali kwa
sababu siyo nyaraka halali za MUWAWATA vile vile nyaraka zilizosambazwa
kupitia mitandao yao ya kijamii pia ni batili,taarifa zilizosambazwa za
kufanyika Mkutano uwanja wa ndani wa Taifa tarehe 3,Augost,2013 siyo za
MUWAWATA na mkutano huo siyo halali,uongozi wa MUWAWATA bado
unawasiliana na serikali ili kuweza kupata majibu ya malalamiko ya
ufinyu wa pensheni ya Wastaafu kwani bado serikali inatujali juu ya
suala hilo”,alisema Mayungi.
Post a Comment