Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mkuu mstaafu Augustino
Ramadhani (aliyesimama) akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la
Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara katika mkutano
ulioitishwa na Tume ili kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba
Mpya wakati wa mkutano uliofanyika Wilayani humo hivi karibuni. Kulia ni
Mjumbe wa Tume, Bw. Yahya Msulwa.
Mjumbe
wa Baraza la Katiba la Halmshauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya, Bw.
Tata Kibona akiwasilisha maoni ya wajumbe wenzake waliojadili eneo la
maadili katika Rasimu ya Katiba Mpya iliytotolewa na Tume ya Mabadiliko
ya Katiba katika mkutano uliofanyika hivi karibuni.
Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Salma Maoulidi (kulia) akizungumza
na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani
Kilimanjaro katika mkutano ulioitishwa Tume wa kuijadili na kuitolea
maoni Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume hiyo. Kushoto ni Mjumbe
wa Tume, Profesa Mwesiga Baregu.
………………………………………………………………………..
TUME
ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwakumbusha wananchi kuwa mwisho wa
kupokea maoni kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kutoka kwa asasi, taasisi, na makundi ya watu yenye malengo
yanayofanana ni siku ya Jumamosi, tarehe 31 Agosti 2013.
Tarehe
31 Agosti, 2013 ilipangwa na kutangazwa katika Mwongozo Kuhusu Mabaraza
ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu Wenye Malengo
Yanayofanana uliotolewa na Tume na ulianza kutumika tarehe 01 Juni 2013.
Utaratibu wa Kuwasilisha Maoni
Kwa
mujibu wa Aya Na. 4.0 ya mwongozo huo, Asasi, Taasisi na Makundi ya
Watu wenye Malengo yanayofanana yanatakiwa kuwasilisha kwa Tume maoni
hayo kwa njia ya randama, barua, andiko au muhtasari wa makubaliano,
n.k.
Hivyo basi
Asasi, Taasisi au Makundi ya watu wenye Malengo yanayofanana yanaweza
kupeleka maoni yao moja kwa moja katika ofisi za Tume zilizopo jijini
Dar es Salaam, Mtaa wa Ohio au Zanzibar, Mtaa wa Kikwajuni, Gofu Jengo
la Mfuko wa Bararabara. Aidha, wanaweza kutuma maoni hayo kwa kutumia
barua pepe ambayo ni katibu@katiba.go.tz au anuani zifuatazo:
- Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 1681, Dar es Salaam; au
- Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 2775, Zanzibar.
Muda wa Kuwasilisha Haujaongezwa
Tume inapenda kusisitiza kuwa muda wa kupokea maoni kuhusu Rasimu ya Katiba haujaongezwa na kuwa Asasi, Taasisi na Makundi ya watu wenye Malengo yanayofanana kuzingatia tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maoni iliyopangwa na Tume.
Post a Comment