|
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
WILAYA YA MBOZI – MAUAJI
MNAMO TAREHE 13.08.2013 MAJIRA YA
SAA 07:00 HRS UKO KIJIJI CHA NANSAMA KATA YA ISANSA WILAYA YA MBOZI MKOA WA
MBEYA. SIJAONA S/O HAONGA MIAKA 45, MKULIMA, MNYIHA, MKAZI WA NANSAMA ALIKUTWA
AKIWA AMEUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO KISHA KUTUPWA KATIKA MTO MLOWO NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI MGOGORO WA MASHAMBA KATI YA MAREHEMU
NA SHABANI S/O MBWILI PAMOJA NA MAWAZO S/O MBWILI AMBAO WALITOROKA MARA BAADA
YA TUKIO HILO. MAREHEMU ALIVIZIWA
WAKATI AKIVUA SAMAKI NA PEMBENI YA MWILI WAKE KULIKUTWA NDOANO.
MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOJICHULIA SHERIA MKONONI NA KUITATUA
MIGOGORO YAO KWA NJIA YA
MAZUNGUMZO NA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WALIOHUSIKA NA
TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.
WILAYA YA CHUNYA – MAUAJI
MNAMO TAREHE 13.08.2013 MAJIRA YA
SAA 00:05 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANGA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. MARIA D/O MARTIN, MIAKA 37, MNYAMWEZI,
MKULIMA, MKAZI WA KANGA ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI KICHWANI NA KUKABWA SHINGONI
NA MPENZI WAKE AITWAE LAMECK S/O MSANGAWALE, MIAKA 35, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI
WA KANGA. CHANZO NI WIVU WA
KIMAPENZI BAADA YA MTUHUMIWA KUMKUTA MAREHEMU AKIWA NA MWANAUME MWINGINE.
MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUYATATUA
MATATIZO YAO YA KIJAMII KWA NJIA YA MEZA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUSHA MATATIZO
YANAYOWEZA KUJITOKEZA. PIA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA ALIYEHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 13.08.2013 MAJIRA YA
SAA 11:00HRS HUKO MAENEO YA UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA WALIMKAMATA IBRAHIMU S/O MATSON ,MIAKA 25,MUWANJI MRISTO NA MKAZI WA
IGAWILO AKIWA NA BHANGI KETE 8 SAWA NA GRAMU 40 NDANI YA MFUKO WA SURUALI . MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI
HIYO .TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|
on Wednesday, August 14, 2013
Post a Comment