Kambi ya upinzani
bungeni imesema kutokana na mtafuruku uliotokea bungeni kwa kutolewa nje
kiongozi wa kambi hiyo Mh. Freeman Mbowe amesema hawaungi mkono muswada wa
sheria ya marekebisho ya katiba ya mwaka 2013 kwa kuwa haiwatendei haki
watanzania.
Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari katika
ukumbi wa Pius Msekwa bungeni mjini Dodoma kuhusiana na mtafuruku uliotokea
bungeni kiongozi huyo wa kambi ya upinzai bungeni Mh Freeman Mbowe amesema
hawatashiriki katika mjadala huo kwa kile walichodai kuwa chama cha mapinduzi
(CCM) kina ajenda ya siri na kushiriki kwao hawatakuwa wanawatendea haki
watanzania
Akizungumzia juu ya kile kinachoonekana kwa sasa kuwa
ni uhusiano mwema baina ya chama cha wananchi (CUF) na Chadema,mbunge wa
Mkanyageni kupitia CUF Mh Habib Mnyaa amesema siasa haina adui wala rafiki wa
kudumu na hivo wameungana na Chadema katika kutetea haki,usawa na maslahi ya
wananchi wa Zanzibara na wale wa Tanzania Bara
Katika tukio jingine
wanasheria wa masuala ya haki za binadamu wamesema kilichotokea bungeni ni
kutokana na kitendo cha naibu spika kuchelewa kutoa majibu ya miongozo kama
ilivyoombwa na baadhi ya wabunge na kuwafanya wabunge wa upinzani kuona
wanaburuzwa na kuamua kutoka nje na kuongeza kuwa hawakufurahishwa na jambo hilo
kwa kile alichodai kuwa mawazo yawachache yanapigwa kumbo
Post a Comment