Kwa kiasi kikubwa, vijiwe husababishwa na kukosekana kwa usawa wa maji,
madini na tindikali mwilini, ambayo kitaalam huitwa electrolyte
imbalance.
FIGO YENYEWE NDIYO HII.
Ni tatizo ambalo linasumbua wengi lakini ambalo halifahamiki vizuri.
Tumesikia habari mbalimbali zinazohusu tatizo hili na dhana mbalimbali ambazo zimekuwa zikijengwa.
Hata hivyo, baadhi ya watu hukumbwa na tatizo la kuwa na vijiwe katika figo na mfumo wa mkojo kwa jumla.
Mawe haya hutokana ama madini, chumvi au tindikali
mbalimbali zinazotolewa mwilini. Nchini Tanzania, baadhi ya wagonjwa
hushtuka wakielezwa wana tatizo hili wakidhani labda wamerogwa, ila
jambo la msingi watambue hili ni tatizo la kiafya.
Aina za mawe katika figo
Aina za vijiwe katika figo ni pamoja na vijiwe vya
calcium oxalate, vijiwe vya tindikali ya uriki (uric acid), vijiwe vya
struvite (magnesium, ammonium na phosphate)
Sababu za vijiwe katika figo
Kwa kiasi kikubwa, vijiwe husababishwa na
kukosekana kwa usawa wa maji, madini na tindikali mwilini, ambayo
kitaalamu huitwa electrolyte imbalance.
Kuna magonjwa kadhaa ambayo husababisha kwa kiasi
kikubwa kutokea kwa hali hii kama ugonjwa wa utindikali kwenye mirija ya
figo, matatizo kwenye tezi za shingo, kukojoa chumvi chumvi za oxalate
kupita kiasi na hali ya nyama za figo kuwa tepetepe.
Nani yupo hatarini?
Tatizo hili huwapata zaidi watu walio na historia
ya familia zao kuwa na vijiwe kwenye figo, walio na umri kuanzia miaka
40 au zaidi, ingawa tatizo hili linaweza kutokea katika umri wowote.
Pia, linaweza kuwapata wanaume zaidi kuliko
wanawake, wana upungufu wa maji mwilini, kwa lugha rahisi wale
wasiopenda kunywa maji katika kiwango kinachoshauriwa. MWANANCHI.
Post a Comment