MAMLAKA
ya Hifadhi ya Ngorongoro imeanzishwa kisheria kama Eneo la matumizi
mseto ya ardhi ikiwa na shughuli tatu kuu. Shughuli hizo ni:
- 1. Uhifadhi wa maliasili katika Eneo la Hifadhi;
- 2. Kuendeleza wenyeji na shughuli zao za ufugaji;
- 2. Kuendeleza utalii.
Katika
shughuli za kuendeleza utalii, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro hutoa
maeneo ya uwekezaji wa mahoteli, kambi za kudumu na kambi za msimu za
kulala wageni.
Kumekuwepo
na taarifa potofu kwenye vyombo vya habari kuhusu ugawaji wa vitalu
kwenye Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Taarifa hizi ni potofu kwa
kuwa Mamlaka haihusiki na ugawaji wa vitalu. Jukumu hilo ni la Idara ya
Wanyamapori.
Aidha,
katika taarifa zilizolipotiwa, Kampuni ya Leopard Tours imetajwa kupewa
kitalu, jambo ambalo siyo kweli. Leopard Tours imepewa “Special
Campsite” ambayo amekuwa akiitumia siku zote – Ndutu Extra kutoka mwaka
2005 hadi sasa. Alikuwa akiitumia kama “Season Campsite” kwa zaidi ya
miezi 5 – 8 kwa mwaka.
Kilichofanyika
ni kuipatia nafasi zaidi Leopard Tours itumie kambi husika kama
“special campsite”. Uamuzi huu ulizingatia kuwa Kampuni hii ni mdau
mkubwa wa shughuli za uhifadhi kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
kwani pato la Mamlaka huchangiwa kwa asilimia kumi (10%) na Kampuni hiyo
ikifuatiwa na Kampuni ya Ranger Safari ambayo huchangia asilimia sita
(6%). Kwa maana nyingine Leopard Tours ndiyo kampuni inayoleta wageni
wengi Hifadhi ya Ngorongoro kulinganisha na Kampuni nyingine
zinazochangia. Kampuni nyingine zinachangia asilimia tatu (3%) hadi
0.13% kwa mwaka.
Aidha
ieleweke kuwa, kwa mujibu wa taratibu za uwekezaji za Mamlaka, eneo
lenye ukubwa wa ekari kumi ambalo alipaswa kupewa mwekezaji Fazal wa
Leopard Tours lilipaswa kulipiwa kiasi cha dola elfu sitini (60,000),
hata hivyo Fazal alipewa eneo linalokaribiana na nusu ya eneo
alilostahili kupewa.
Kutokana
na hilo, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iliamua mwekezaji huyo alipe
nusu ya pesa aliyopaswa kulipa ambayo ni dola za Marekani elfu
thelathini (30,000).
Hivyo basi Mamlaka inasisitiza kuwa taarifa zilizolipotiwa kwenye vyombo vya habari kukusu mwekezaji huyu zilipotoshwa.
KAULI MBIU YETU
“UTALII UANZE NA MTANZANIA KWANZA”
ImetolewanaKaimuMhifadhi
MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO
Post a Comment