Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara amewateua Wajumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspapers Ltd (TSN)
baada ya bodi ya awali kumaliza muda wake mwishoni mwa mwezi Machi, 2013.
Uteuzi wa Mhe. Waziri unafuatia uteuzi alioufanya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamahuri ya Muungano
wa Tanzania kwa Profesa Moses Wariobi kuwa wa Mwenyekiti wa Bodi ya TSN. Wajumbe wa Bodi ni kama Ifuatavyo:
1. Dkt. Consolata Ishebabi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara
2. Everlyn Richard kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam
3. Alfred Nchimbi, Chuo cha Utumishi wa Umma
4. Glorious Luoga, Mwanasheria
Uteuzi huu ni kuanzia tarehe 6 Septemba, 2013
Post a Comment