Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na
Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye wakishiriki
katika ujenzi wa Birika la Kunyweshea mifugo linalojengwa katika Kata ya
Didia Jimbo la Solwa Katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga vijijini
mkoani Shinyanga, ambapo leo katibu Mkuu huyo ameendelea na ziara yake
ya siku nne mkoani humo na kushiriki katika shughuli mbalimbali za
maendeleo katika kuimarisha uhai wa chama hicho na utekelezaji wa Ilani
ya ya Uchaguzi.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE -SHINYANGA. 

Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na
Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum wakicheza na nyoka pamoja na
wanakukundi cha utamaduni kutoka jimboni humo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja akimlipa ujira wa shilingi elfu 10.000 Katibu
wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye baada ya kumsaidia
katika ujenzi wa Birika la kunweshea mifugo katika kata ya Didia, hata
hivyo Kinana aliwapa fedha pia wajenzi wa birika hilo. 

Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza
na wananchi wakati alipokagua ujenzi wa Soko la Kata ya Didia
lililojengwa katika kijiji cha Didia, kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mngeja.

Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga
picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mbele ya soko hilo. 

Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akipata
maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Vijijini Bw.Kiyungi Mohamde Kiyungi wakati alipokagua ujeni wa Hospitali
ya Halmashauri hiyo inayojengwa katika kijiji cha Iselamagazi, wa tatu
kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mngeja. 

Katibu
wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akicheza na nyoka
wakati aliposhiriki katika kucheza ngoma ya asili katika kijiji cha
Didia. 

Hili ndilo soko la Didia 

Wapiga
ngoma wa Kikundi cha ngoma cha Didia wakipiga ngoma wakati Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokagua ujenzi wa soko la Didia. 

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi
waliomsimamisha katika kijiji cha Mwabenda ambao walikuwa na mabango
yaliyokuwa yakielezea kero zao katika kijiji hicho ambazo zilikuwa ni
Umeme na maji hata hivyo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ndugu Ally Rufunga
aliwaelezea mipango ya serikali kuhusu kijiji hicho katika kuhakikisha
maji na umeme vinapatikana mapema katika kijiji hicho. 

Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Salawe katika jimbo la Solwa mkoani Shinyanga. 

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtunza mmoja wa wasanii wa
kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbiza katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Salawe katika jimbo la Solwa mkoani Shinyanga. 

Wananchi wakiwa wamehudhuria kwa wingi katika mkutano huo wa hadhara.

MNEC Azza Hilal Hamad kutoka Viti Maalum mkoa wa Shinyanga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kijijini Salawe. 

Mbunge
wa jimbo la Solwa Ahmed Salum akiwahutubia wapiga kura wake katika
kijiji cha Salawe ambapo mkutano wa hadhara umefanyika leo. 

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Salawe ambapo mkutano wa hadhara umefanyika leo.




















Post a Comment