Rais wa
Nigeria Goodluck Jonathan amewafuta kazi mawaziri tisa katika hatua yake
ya kwanza kubwa ya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.
Ni mara
ya kwanza tangu kuchaguliwa miaka miwili iliyopita, kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na msemaji wa serikali hii leo. Hata hivyo taarifa
hii inakuja wakati kuna migawanyiko mikubwa katika serikali
Mawaziri
walioachishwa kazi ni pamoja na waziri wa mambo ya nje, elimu, waziri
wa Sayansi na teknolojia , waziri wa makaazi na ustawi wa miji, waziri
wa mipango ya serikali na mazingira
Mawaziri
wengine waliofutwa kazi ni ule wa mambo ya ndani na manaibu waziri wa
kawi na kilimo pamoja na ulinzi ambao pia waliachishwa kazi.
Taarifa zilisema kuwa mawaziri wapya watateuliwa lakini mara moja.
Wiki
mbili zilizopita magavana saba wenye ushahwishi mkubwa sana pamoja na
aliyekuwa makamu wa rais Atiku Abubakar waliunda vuguvugu lao pakee na
kujitenga na chama tawala
Walighadhabishwa na hatua ya washirika wao kunyimwa fursa ya kugombea nyadhifa za kisiasa katika chama tawala.
Wadadisi wanasema kuwa ugomvi unatokana na wanasiasa kuanza kujipanga au kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
Chama cha
kitaifa kimeshinda uchaguzi wote wa kitaifa tangu mwaka 1999 mwishoni
wa utawala wa kijeshi kwa hivyo kiongozi wa chama ambaye ni Godluck
Jonathan atakuwa na fursa nzuri ya kushinda kwenye uchaguzi huo.
chanzo bbc.


Post a Comment