Katibu Mkuu wa CCM, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amezitaka
ofisi za chama hicho wilayani na mikoani kuhakikisha mikataba yote ya
uchumi ambayo wanaingia inakuwa wazi kwa wanachama.
Akizungmza baada ya kuwasili Nzega, mkoani Tabora
jana, Kinana alisema hatua hiyo itaondoa mikataba hiyo kuwanufaisha watu
wachache.
Kinana aliyasema hayo baada ya kuweka jiwe la
msingi la mradi wa ujenzi wa mabanda 54 kuzunguka Uwanja wa Michezo wa
Samora, unaomilikiwa na chama hicho Wilaya ya Nzega.
Ujenzi huo utakapokamilika mabanda hayo yatakodishwa kwa wafanyabiashara watakaolipa kodi CCM.
Alisema mikataba yote iwe wazi na taarifa zake ziwasilishwe kwenye vikao mahsus, ili wanaotaka kuhoji wafanye hivyo.
Katika hatua nyingine, Kinana alimmwagia sifa
Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangallah, akimtaja kuwa mchapaka kazi
ambaye hachoki, huku wananchi waliohudhuria wakimtaja mbunge huyo kuwa
ni ‘jembe.’
Awali, akisoma taarifa ya mradi huo, Katibu wa
Uchumi na Fedha wa CCM Wilaya ya Nzega, Majaliwa Bilal, alisema mradi
huo unatekelezwa kwa utaratibu wa wafanyabiashatra kujenga vibanda hivyo
kwa gharama zao. MWANANCHI
Post a Comment