Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Musoma mjini katika viwanja vya shule ya msingi Mkendo.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya sanamu ya mfano wake kutoka kwa Ndugu Elia Bugurilo Kamoga.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa anavuka na kivuko cha MV
Musoma kutoka Kinesi kuelekea Musoma mjini,Kivuko hicho ambacho
kimekuwa mkombozi wa usafiri kinauwezo wa kubeba abiria 330.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijaribu vazi la kujiokoa wakati
wa hatari wakati wa kuvuka na kivuko cha MV Musoma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishangiliwa na Balozi wa shina namba 6 Tabitha Edgar wa kata ya Kitagi.
Balozi
wa nyumba kumi Tabitha Edgar wa shina namba 6 kata ya Kitagi akitoa
shurani zake za kutembelewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abbulrahman
Kinana.
Katibu
Mkuu akipata maelezo ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria
uliopo eneo la Bukanga(Makoko) mradi huo utakamilika katikati ya mwaka
ujao.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua maendeleo ya mradi
mkubwa wa maji huku akipatiwa maelezo na mhandisi Jairos Chilema ,mradi
huo utakuwa na bomba kubwa la kilomita tisini na ukikamilika utaondoa
kabisa tatizo la maji Musoma Mjini.
Post a Comment