Meneja
wa Magereza Saccos, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Godfrey Kavishe (wa
kwanza kushoto) akiwatembeza Maafisa na Askari toka JKT Saccos katika
jengo la Saccos ya Magereza walipotembelea leo Septemba 11, 2013 jijini
Dar Es Salaam.
Afisa
Mikopo wa Magereza Saccos, Mrakibu wa Magereza Nahman Koko (wa pili
kushoto) akiwatambulisha Maafisa na Askari toka JKT Saccos kwa
askari Stafu Sajini Naftal Shango(wa kwanza kushoto) anayeshughulika na
Usajili wa wanachama walipotembelea Magereza Saccos leo Septemba 11,
2013 jijini Dar Es Salaam
Meneja
wa Magereza Saccos, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Godfrey Kavishe
(katikati waliovaa sare) akitoa maelezo ya utangulizi kuhusu Chama cha
Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania
Bara kwa Maafisa na Askari toka JKT Saccos walipotembelea leo Septemba
11, 2013 jijini Dar Es Salaam
Baadhi
ya Maafisa na Askari toka JKT Saccos wakiongozwa na Meja Haule (wa
kwanza kulia) wakimsikiliza Meneja wa Magereza Saccos, Mrakibu
Mwandamizi wa Magereza Godfrey Kavishe (hayupo pichani) wakati akitoa
maelezo ya utangulizi kuhusu Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha
Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara walipotembelea leo Septemba
11, 2013 jijini Dar Es Salaam (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la
Magereza). Muonekano
wa mbele wa Jengo la Chama cha Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi
la Magereza Tanzania Bara (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la
Magereza).
Post a Comment