TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 11. 09. 2013.
WILAYA YA RUNGWE - KUTUPA MTOTO MCHANGA.
|
MNAMO
TAREHE 10.09.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO KATIKA MTAA WA BAGAMOYO –
TUKUYU MJINI WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. ILIOKOTWA MAITI YA
MTOTO MCHANGA MWENYE UMRI WA SIKU MOJA JINSI YA KIKE IKIWA IMETELEKEZWA
NA MAMA MZAZI WA MTOTO HUYO AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA. MWILI WA
MAREHEMU AMBAO UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI YA MAKANDANA –
TUKUYU ULIKUTWA NYUMA YA KISIMA CHA MAFUTA CHA CALTEX UKIWA
UMEVINGIRISHWA KWA KUTUMIA KIPANDE CHA KITENGE KISHA KUWEKWA NDANI YA
MFUKO WA RAMBO NA JUU YAKE KUWEKWA JIWE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA ALIYEFANYA KITENDO
HIKI CHA KIKATILI NA CHA KINYAMA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE,VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE
MARA MOJA.
Imesainiwa na
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment