NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
OFISI
ya Uhamiaji mkoa wa Dares Salaam imemfikisha mahakamani Mtanzania
anayedaiwa kuwatunza raia watano kutoka Nigeria wanaoishi nchini bila
kibali halali baada ya kuwapiga na kuwazuia kufanya kazi maofisa wa
uhamiaji kwenye ofisi za Serikali.
Hayo
yalisemwa leo na Ofisa wa Uhamiaji wa Mkoa wa Dares Salaam Grace
Hokororo wakati akizungumza na mwandishi wa Idara ya Habari –MAELEZO
ofisini kwake ambapo alisema Mtanzania huyo alifikishwa leo(jana)
katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu baada ya kutenda kosa hilo
jana majira ya saa 1:00 jioni.
Alimtaja
Mtanzania huyo kuwa ni Christopher Kanyala mwenye umri unaokadiriwa
kuwa kati miaka 29 hadi 34 mkazi wa Sinza na anadaiwa kuwa
aliwakutumikia Jeshi la Polisi nchini, ambapo kesi yake na raia hao
watano wa Nigeria itatajwa kesho katika mahakama hiyo.
Akizungumzia
kuhusu suala hilo , Grace aliwataka wananchi wasipende kuishi na raia
ambao ni wageni na hawajaripoti katika ofisi za uhamiaji kwa kufanya
hivyo ni kosa kisheria. Huku akiwataka raia wa kigeni kuripoti katika
ofisi hizo mara baada ya kuwasili nchini ili waweze kufuata taratibu
za kisheria.
Aidha alisema operesheni ya kuwakamata wahamiaji haramu inaendelea vizuri.
Grace
alisema kwa upande wa wahamiaji haramu kutoka Malawi walijitokeza kwa
hiari mpaka leo mchana idadi yao imefikia 1,863 tangu zoezi hilo
lilipoanza.
Aliongeza
kuwa opresheni hiyo imehusisha mataifa 31 ambapo alitaja baadhi yake
kuwa ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda,Italia, Singapore Ethiopia,Libya
Yemeni,Somalia,Komoro, Ujerumani, Afrika Kusini,Uturuki, Nigeria,
Cameroon,Liberia na Bokinafaso., Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo(DRC) na
India.
Alisema jumla ya raia hao wa mataifa mengine waliokamatwa ni 502.



Post a Comment