
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge taifa Juma Ali Simai akimueleza jambo Mke wa Rais
ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Mama Salma Kikwete
wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru yaliyofanyika leo katika eneo
la Mto Mkavu – Mbanja kutoka Halmashauri ya wilaya ya Lindi kwenda
Manispaa ya Lindi. 

Kiongozi
wa Mbio za Mwenge taifa Juma Ali Simai akimkabidhi Mwenge wa Uhuru
mkimbiza mwenge namba moja katika manispaa ya Lindi Mke wa Rais ambaye
pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Mama Salma Kikwete wakati
mwenge huo ulipowasili leo katika eneo la Mto Mkavu – Mbanja. Wapili
kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Dk. Mohamed Nassor. 

Mkimbiza
Mwenge namba moja katika manispaa ya Lindi Mke wa Rais ambaye pia ni
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Mama Salma Kikwete akisalimiana na
Mbunge wa Mchinga Said Mtanda wakati mwenge huo ulipowasili leo katika
eneo la Mto Mkavu – Mbanja. Kiongozi wa Mbio za Mwenge taifa Juma Ali
Simai (hayupo pichani) alipongeza Mbunge huyo kutokana na moyo wake wa
kujitoa na kushiriki katika mbio za mwenge mkoani Lindi na kuwataka
wabunge waige mfano. 

Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Taifa Juma Ali Simai akimkabidhi Mwenyekiti wa klabu
ya kupinga rushwa katika chuo cha Ufundi VETA kilichopo Manispaa ya
Lindi Abdallah Makwinya kifurushi chenye nakala mbalimbali zinazoeleza
jinsi ya kupambana na rushwa chuoni hapo.Kushoto ni Mkimbiza Mwenge
namba moja katika manispaa ya Lindi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. 

Afisa
kutoka Ofisi ya TAKUKURU mkoani Lindi Amos Ndege akielezea umuhimu wa
klabu ya kupinga rushwa iliyopo katika chuo cha Ufundi VETA jinsi
itakavyosaidia kutoa elimu kwa vijana. Wanaomsikiliza kwa makini ni
Mkimbiza Mwenge namba moja katika manispaa ya Lindi Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete akifuatiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Taifa Juma Ali
Simai. 

Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Taifa Juma Ali Simai akifungua darasa litakalotumiwa
na klabu ya kupinga rushwa katika chuo cha Ufundi VETA kilichopo
Manispaa ya Lindi kwa ajiili ya kutoa elimu kuhusiana na madhara ya
rushwa kwa jamii. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Dk. Mohamed Nassor. 

Viongozi
wa Serikali na vyama vya siasa wa manispaa ya Lindi wakijiandaa
kuupokea Mwenge wa Uhuru kutoka wilaya ya Lindi zoezi hilo limeafanyika
leo katika eneo la katika eneo la Mto Mkavu – Mbanja. Ukiwa katika
Manispaa ya Lindi Mwenge huo utafungua, kuzindua na kuweka mawe ya
msingi katika miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni
1.5.
Wakimbiza
Mwege Taifa, Viongozi wa Serikali wa wilaya ya Lindi na Askari Polisi
wakielekea kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa viongozi manispaa ya Lindi
zoezi hilo limefanyika leo katika eneo la Mto Mkavu – Mbanja
Picha na Lorietha Laurence – Maelezo


Post a Comment