Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS DKT. SHEIN AZINDUA MADARASA CHUO CHA SAYANSI YA AFYA MBWENI

 


IMG_4011
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,Dk.Haji Mwita,alipotembelea Dagfhalia ya Wanafuzi wa Chuo hicho kabla ya kuzindua  madarasa ya Chuo hicho leo huko Mbweni nje ya Mji wa Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] 
IMG_4045
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni  Nje ya Mji wa Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_4053
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,wakikata utepe kama ishara ya ya uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni  Nje ya Mji wa Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] 

IMG_4084  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa ushauri wakati alipotembelea moja ya madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,huko mbweni baada ya kuyazindua rasmi leo,ambayo yamejengwa kwa ufadhili ya Serikali ya Oman kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] 
IMG_4126
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa nasaha zake,baada ya kuyazindua rasmi madarasa ya chuo hicho leo ,hapo chuoni Mbweni,Mkoa wa Mjini Mgharabi  Nje ya Mji wa Unguja, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] IMG_4132
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea risala ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Dk. Haji Mwita,baada ya kuyazindua Rasmi madarasa ya Kusomea,yaliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Oman,na ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_4153
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa hutuba yake kwa
Wananchi na wanafunzi (hawapo pichani) wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa jengo la madarasa  ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Oman kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,huko Mbweni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo,(kushoto) Waziri wa Afya Juma Duni Haji,na Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,(kulia).[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] 
IMG_4140
Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,akitoa salamu
zake wakati wa sherehe za uzinduzi wa madarasa mapya ya kusomea katika Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,yaliyojengwa na  Serikali ya Oman,na ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top