Mchumba wa Dk. Slaa Josephin Mushumbuzi akiwa na mmoja wa mwekezaji wa kijapan. |
Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema, Dr. Slaa anapenda
sana kujinasibisha kwamba yeye ni mzalendo wa kupindukia, anayechukia
vitendo vya ufisadi na anayeionea huruma nchi yetu.
Taarifa za
uhakika kabisa zinathibitisha kwamba mwishoni wa mwezi Juni, mwaka 2013
Dr.Slaa na Mchumba wake walitembelewa na kundi la Wajapani wapatao 20
nyumbani kwao Mbweni, Kinondoni ambapo wote kwa pamoja walikula cha
jioni.
Dhumuni la ugeni huo wa Wajapani, ilikuwa ni
kuthibitisha kama kweli Chadema kina mpango wa kujenga hospitali kubwa
ya kisasa katika eneo la Mlalakuwa Dar es Salaam, Wajapani hao ndiyo
walipangwa au kuteuliwa kujenga hospitali hiyo, wameakikishiwa pamoja na
mambo mengine ya kimaslahi yao makampuni yao mengine, kwamba msimamizi
wa hospitali hiyo ndiyo atakayekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania mwaka 2015, kwa maana ya Dr. Slaa.
Mipango yote ya
kujenga hospitali hiyo, inaratibiwa na Askofu mmoja anayemiliki Kanisa
lake maeneo ya Kawe, Dar es Salaam, Askofu huyo amekuwa akifanya safari
za Japani akiwa ameandamana na mchumba wa Dr. Slaa, Josephine, mpango
unafanyanyika vifaa vyote vitakavyoingizwa kutoka Japani vipitie
mikononi mwa Kanisa ili tu visitozwe kodi na serikali. CHANZO: IDEOLOGICAL FORUM-FACEBOOK
on Tuesday, September 10, 2013
Post a Comment