Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waziri mkuu Mhe. Pinda aongoza ufunguzi wa maonesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China

 


picha no.1
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kulia) akikata utepe leo kuashiria ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini  China yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne yanalengo la kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini humo ili viwanda na makampuni ya nchi hiyo waweze kufanya biashara na watanzania. Kulia kwa waziri mkuu ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda na kushoto kwake ni Balozi wa China nchini LV Youqing. picha no.2
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alijaribu jembe la kupandia nafaka wakati alipotembelea banda la kiwanda cha Qingyuan  Manchu Autonomous County cha nchini China wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini humo yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Wanaomtazama ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda (kushoto)  na  Balozi wa China nchini LV Youqing (kulia). picha no. 3
Mfanyakazi wa kiwanda cha Changzhou Amec Group cha nchini China Yan Xing Long (kulia) akimueleza Waziri Mkuu Mizengo Pinda jinsi mashine ya kuchanganya kokoto iliyotengenezwa na  kiwanda hicho  inavyofanya kazi  wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini humo yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
  picha no. 4
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia mfano wa nyumba zinazojengwa na kampuni ya Beijing New Building Material alipotembelea banda hilo wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China  yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wapili kulia  ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda na watatu kushoto ni Meneja Msaidizi Idara ya Biashara ya Kimataifa  wa Kampuni Alec Lu. picha no. 5
Baadhi wa watu mbalimbali walioshiriki  ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China  yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne ambayo yamefunguliwa leo yanalengo la kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini humo ili viwanda na makampuni ya nchi hiyo yaweze  kufanya biashara na watanzania.
picha no.6
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia malighafi zinazotumiwa na  kampuni ya  Beijing New Building Material kutengenezea nyumba alipotembelea banda hilo leo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China  yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wa kwanza  kushoto ni Meneja Msaidizi Idara ya Biashara ya Kimataifa  wa Kampuni hiyo Alec Lu na wapili kulia ni Makamu Meneja Mkuu Fred Yu. PICTURE NO. 7
Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda (katikati) akiongea na viongozi kutoka nchini China leo wakati wa sherehe za ufunguzi wa maonyesho  ya bidhaa zinazozalishwa nchini  humo yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top