Waziri
wa wa nchi Ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais Bi. Fatma Abdulhabib
Fereji akizindua bodi mpya ya makamishna wa tume ya ukimwi zanzibar
kwenye ofisi ya tume ya ukimwi shangani.
NA RAMADHANI ALI / HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Waziri
wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej leo
amezindua Bodi mpya ya Makamishna wa Tume ya Ukimwi Zanzibar na kuitaka
kushirikiana kwa karibu zaidi na wadau mbali mbali kuanzia ngazi ya
chini ili kuhakikisha maambukizi ya janga la Ukimwi yanapungua na
kufikia lengo la Zanzibar bila Ukimwi inawezekana.
Waziri
Ferji amewaeleza wajumbe hao kwamba Ukimwi ni janga la Taifa, na
mapambano ya ya gonjwa hilo yamejaa changamoto nyingi ambazo zinahitaji
kufanyiwa kazi kwani bado wapo watu hawataki kuelewa ingawa juhudi
kubwa za kuwaelimisha zimechukuliwa.
Katika
kuanza kazi zake, Waziri wa Nchi Afisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais
ameieitaka safu mpya ya Makamishna kufanya ziara za mara kwa mara sio
katika maofisi tu bali kuwapitia wadau kujua changamoto zinazowakabili
kwa lengo la kunagalia namna Tume inavyoweza kusaidiana nazo katika
kuzitatua.
“Hilo
ni jambo muhimu sana na tukifanya hivyo tutaweza sote kujiridhisha na
yale tunayojipangia kuyatekeleza katika mipango yetu ya mwaka au robo
mwaka,”alisisitiza Waziri Fatma Abdulhabib Ferej.
Amewashauri
Makamishna wapya katika kipindi cha miaka mitatu ya kazi, kuendelea
kuwa karibu zaidi na watendaji na Wafanyakazi wa Tume katika kusimamia
utendaji na uwajibikaji ili kufikia lengo la kuanzishwa sheria namba 3
ya mwaka 2002 ya Tume ya Ukimwi Zanzibar.
Amesema
kwa upande wake na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa jumla wapo
tayari kutoa kila msaada kwa Tume kila itapohitajika ili kufanikisha
kazi zao kwa ufanisi mkubwa.
Ameeleza
matumaini yake kuwa kutokana na Tume hiyo mpya kusheheni Makamishna
wenye uzoefu mkubwa na shughuli za Bodi na mapambano dhidi ya ukimwi
hategemei kama shughuli zitazozorota.
Amewapongeza
wajumbe waliomaliza muda wao kwa namna walivyoisaidia Tume ya Ukimwi
licha ya changamoto nyingi walizokabiliana nazo lakini busara zao na
uwezo wao umesaidia sana ufanisi katika shughuli za Tume.
‘Ni
imani yangu ya dhati kwamba mafanikio yaliyopatikana ndani ya Tume
yametokana na michango yao kutokana na uzoefu wao pamoja na maelekezo
yao, ’alisema Waziri Ferej.
Alitaja
moja ya fanikio la kujivunia kwa Makamishna hao ambalo ni la kupigiwa
mfano ni kwamba wakati baadhi ya nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara
wamefikia kiwango cha maambukizo cha asilimia kati ya ishirini na
thelathini katika miaka ya hivi karibuni, Zanzibar imeweza kudhibiti
kiwango cha maambukizo chini ya asilimia moja.
Amewaomba
wajumbe hao kuwa tayari kuendelea kuisaida Tume mpya kila
watakapohitajiwa kufanya hivyo kwa vile ni watu wenye uwezo mkubwa
katika kusaidia maendeleo ya Tume ya Ukimwi.
Katika
uzinduzi wa Bodi uliofanyika Tume ya Ukimwi Shangani, limpongeza
Mwenyekiti aliemaliza muda wake Professa Saleh Idrissa Mohammed kwa
kuteuliwa tena na Rais kwa kipindi chengine cha miaka mitatu na kueleza
kuwa ni kutokana na uwezo wake mkubwa alioonyesha katika kuiongoza Bodi
hiyo.
Kwa
upande wake Professa Idrissa amemuhakikishi Waziri kwamba watatekeleza
wajibu wao waliokabidhiwa na Taif na kuhakikisha huduma za Tume
zinawafikia wananchi wote na kufikia lengo la kuhakikisha janga la
ukimwi linapungua kwa kiasi kikubwa na vizazi vijavyo visome historia
kuwa kulikuwa na Ukimwi Zanzibar.
Makamishna
wapya wa Tume ya Ukimwi Zanzibar ni Abeid Saad Said kutoka Taasisi
zisizo za Kiserikali, Sheikh Mziwanda Ahmed Taasisi za Dini, Hasina
Hamad kutoka vyombo vya Habari, Munira Humud Taasisi za Biashara na
mjumbe mmoja kutoka Jumuiya ya watu wanaoishi na Viruza vya ukimwi
Zanzibar.
Wajumbe
wanaoingi moja kwa moja kwa mujibu wa nyadhifa zao ni Makatibu Wakuu
wa Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya, Wizara ya Vijana, Wanawake na watoto
na Uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na Wizara ya Tawala za Mikoa na
Vikosi vya SMZ.



Post a Comment