Marehemu Julius Nyaisangah
(katikati) akiwa katika pozi na Meneja Mkuu wa Global Publishers
Abdallah Mrisho (kushoto) na Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Uwazi Elvan
Stambul (kulia) walipokuwa katika semina ya wanahabari Bagamoyo mwaka
2011.
*******
Mtangazaji wa siku nyingi Tanzania Julius Nyaisanga amefariki dunia leo asubuhi.Nyaisanga alipelekwa hospitali ya Mazimbu Morogoro jana saa nane mchana kutokana na kusumbuliwa na Kisukari pamoja na presha ambapo asubuhi ya leo October 20 2013 ndio akafariki dunia.
Mara yake ya mwisho kuingia ofisini ilikua juzi japo alikua ameanza likizo toka October 12 ambapo huu ulikua ni mwaka wake wa tatu toka ameanza kufanya kazi na Abood Media ya Morogoro kama Meneja wa kituo.
Taarifa nyingine kuhusu msiba wake utaendelea kuzipata hapa millardayo.com
R.I.P Uncle J.J


Post a Comment