Watu wawili mkoani hapa wameuawa kikatili mmoja kwa kuchomwa moto na mwingine kuchinjwa kama kuku.
Aliyechomwa moto anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 baada ya wananchi kumtuhumu kuiba kuku wanne.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani
Shinyanga, Kamishina msaidizi wa polisi, Evarist Mangala, alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa wananchi hao walimshambulia
kijana huyo kwa kumpiga mawe, fimbo, marungu na kuuchoma mwili wake.
Katika tukio lingine Lucia Masunga (61),
mkazi wa kata ya Kizumbi mjini hapa, aliuawa na watu wasiojulikana kwa
kumchinja shingo na kusababisha kifo chake hapohapo.
Mwanamke huyo alivamiwa juzi majira ya saa
4 usiku akiwa nyumbani kwake wakati akijiandaa kula chakula cha usiku
na ndipo alipovamiwa na watu wasiojulikana na kisha kumchinja shingo na
kusababisha kifo chake.
Kamanda Mangala alisema chanzo cha mauaji
ya tukio la kwanza ni marehemu kutuhumiwa kuiba kuku na katika tukio la
pili jeshi bado linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo.
CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI



Post a Comment