Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BUNGENI KWALIPUKA TENA






*Wabunge wa Upinzani, CCM wakamianaWAKATI Bunge likitarajia kuanza kuketi kesho, huku kukiwa na taarifa za kurudishwa kwa hati ya dharura Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya kuifanyia marekebisho, joto la mjadala wa kuipitia upya sheria hiyo limeanza kupanda miongoni mwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa vyama vya upinzani.

Kauli ambazo zimeonekana kutolewa sasa na wabunge wa pande zote mbili wakati wakizungumza na gazeti hili kuhusiana na hatua hiyo ya kuirudisha bungeni sheria hiyo iliyosainiwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete, inatoa taswira kwamba huenda ukazua mpasuko mkubwa kuliko ule wa mwanzo endapo kutatokea upande mmoja kutokubali hoja za upande mwingine.



Rai Jumapili lilifanya mahojiano kwa nyakati tofauti na baadhi ya wabunge wa vyama mbalimbali, ambao wametoa kauli za kusigana zinazoashiria kwamba kama hakutatumika busara ya ziada katika vikao vya kupitia marekebisho ya sheria hiyo, Bunge linaweza kuparaganyika.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), aliliambia gazeti hili kuwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inaweza kupita salama katika majadiliano ya kusahihisha mapungufu yaliyosababisha mpasuko miongoni mwao katika Bunge lililopita, lakini akaonya kwa kusema mafanikio hayo yatakuja kama wabunge wa CCM wataacha ushabiki na wendawazimu wa kupinga hoja za msingi zinazotolewa na wabunge wa upinzani.

“Wabunge wa CCM kama wataondoa wendawazimu wao wa kupinga hoja za mashiko zinazotolewa na wabunge wa upinzani, basi Muswada huu utapita bila matatizo, lakini wakiendelea na uwendawazimu wao wa siku zote, hakika hatutakubali na kutatokea vurugu kubwa…sisi tunataka hoja zetu zisikilizwe na kisha tuelewane,” alisema Mchungaji Msigwa.

Katika hatua nyingine, Mchungaji Msigwa alimsifu Rais Jakaya Kikwete kwa kuyabaini mapungufu na kuamua kuirudisha bungeni sheria hiyo kwa marekebisho, hatua ambayo inatoa fursa kwa wabunge wa vyama vyote kufikia makubaliano yenye usawa ili sheria iweze kusimamia Katiba yenye manufaa kwa Watanzania wote.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendaradi Kigola (CCM), alisema kwamba anaamini katika hoja zenye maslahi kwa taifa, lakini kama wabunge wa upinzani watatoa hoja zenye manufaa kwao na si utaifa hakuna mbunge yeyote wa CCM ambaye atakubaliana nazo.

Alisema Bunge ni chombo chenye mamlaka kamili, hivyo si kwamba hoja zote za wabunge wa upinzani zitakubaliwa kwa sababu muswada huu ni nyeti sana katika kutuzalishia sheria ya Katiba Mpya, hivyo kuna haja ya kuwapo kwa tathimini kuhusu mapendekezo ya wapinzani na yale yenye mashiko kwa Watanzania wote ndiyo yatapitishwa na wabunge wote, lakini si kila pendekezo wanalolitoa wapinzani ni lazima lipitishwe.

“Hakuna mtu wa kukubali hovyo mapendekezo yasiyo na utaifa, sisi kama wabunge kazi yetu ni kutunga sheria kwa ajili ya Watanzania wote, hivyo kama mapendekezo watakayoyawasilisha wapinzani yatakuwa na manufaa kwa taifa, hatutayapinga,” alisema Kigola.

Naye, Mbunge wa Kasulu Mjini, Mosses Machali (NCCR-Mageuzi), alisema kurudishwa kwa mara nyingine Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, kunadhihirisha kwamba wabunge wa CCM wanapenda kushabikia madudu.

Alisema lengo la wabunge wa CCM ni kuuchelewesha mchakato wa Katiba, hali ambayo inaonesha ni hujuma dhidi ya mwenyekiti wao Rais Kikwete ambaye nia yake ni kuhakikisha anaondoka madarakani huku akiacha jambo la kukumbukwa la kuzaliwa kwa Katiba Mpya.

“Najua wabunge wa CCM watakuwa wamekaa na viongozi wao kwa ajili ya kuujadili muswada huu, nawaomba watumie busara, hakuna mtu atakayekubali kuburuzwa, wakizipinga hoja zetu nasi tunaususia kwa mara nyingine muswada huo,” alisema Machali.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy, alisema anashindwa kuelewa sababu ya ukimya wa viongozi wa vyama vya upinzani waliokwenda Ikulu kuonana na rais, hivyo kueleza kwamba huenda viongozi hao wakawa na jambo lililojificha nyuma.

Kwa upande wake Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA), Godbless Lema aliwataka wabunge wa CCM wasijisikie wanyonge baada ya Rais Jakaya Kikwete kuchukua uamuzi wa kuurejesha muswada huo bungeni kwa ajili ya marekebisho ya sheria hiyo, kwa sababu hali hiyo inatokana na makosa waliyoyatenda wao wenyewe.

“Najua fika wabunge wa CCM wanajisikia vibaya kwa kurejeshwa kwa muswada huu bungeni, waachane na kinyongo hicho na wajue kwamba hawana ubavu wa kupinga mapendekezo ya wabunge wa upinzani, kwa hiyo nina imani kwamba, mjadala utakuwa shwari,” alisema Lema.

Hivi karibuni viongozi wa upinzani walitoa mapendezo mazito siku chache baada ya vyama vyenye uwakilishi wa wabunge kukutana na Rais Jakaya Kikwete kuzungumzia upungufu katika sheria ya marekebisho ya mabadiliko ya Katiba.

Mapendekezo hayo ya wapinzani mengi yanadaiwa kuwa ni yale yaliyokataliwa na wabunge wa CCM wakati wakipitisha muswada huo bungeni.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top