
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza Rais Mstaafu wa Shirikisho la Mpira
nchini (TFF) Leodger Tenga kwa uongozi wa kutilia mfano uliowezesha
kuleta mapinduzi makubwa ya mifumo ya soka nchini.
Aidha
CCM inamtumia salam za pongezi za dhati Rais Mpya wa TFF, Jamal
Malinzi, na Uongozi wake wote mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
uliopatikana katika uchaguzi uliofanyika juzi, Oktoba 27, 2013 jijini
Dar es Salaam.
Chama Cha Mapinduzi, kinaimani
kubwa na Malinzi wa wenzake katika kuendeleza jitihada zilizoanzishwa na
uongozi uliomaliza muda wake sanjari na kuibua mbinu mpya
zitakazoboresha na kuleta mapinduzi makubwa ya soka nchini.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye anawaasa“Tunauomba
uongozi mpya kujiepusha na jitihada za kujiendeleza binafsi na badala
yake uwekeze katika soka na kuepusha migogoro isiyo na tija katika
mchezo huo ambao kwa sasa ndio unaopendwa na Watanzania wengi”
“Daima imani huzaa imani, hivyo imani ya CCM kwako na kwa viongozi wenzako mliochaguliwa pamoja izae imani ya utumishi uliotukuka” Ndugu Nape amehitimisha.
“Daima imani huzaa imani, hivyo imani ya CCM kwako na kwa viongozi wenzako mliochaguliwa pamoja izae imani ya utumishi uliotukuka” Ndugu Nape amehitimisha.
Chama
Cha Mapinduzi kinatambua kuwa migogoro imekuwa kwa sehemu kubwa chanzo
cha kukwamisha sana maendeleo ya soka hapa nchini na hivyo kuwanyima
Watanzania raha ambayo huitarajia kutoka kwenye mchezo huo na hasa pale
timu zao zinapopata ushindi.
Imetolewa na:-
Kitengo cha Mawasiliano na Umma
Chama Cha Mapinduzi
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu


Post a Comment