Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA CHAONGEZA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2013/2014

 


IMG_8278
Afisa Uhusiano wa Chuo cha Serikali za mitaa Bw.Sebera Fulgence akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na kufanya mafunzo kwa Watumishi wa Serikali  wapatao 4,913,wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano toka Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Bi. Rebecca Kwandu.
Picha na Eliphace Marwa-Maelezo
……………………………………………………………………………..
Chuo cha Serikali za Mitaa [The Local Government Training Institute] Hombolo , Dodoma kimedahili Wanafunzi 1603 kwa mwaka wa masomo 2013/2014. Idadi hii inajumuisha Wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na kujiunga na Astashahada (Basic Technician Certificate courses) na kidato cha sita wanaojiunga na Stashahada (Ordinaly Diploma Courses) katika fani za Uhasibu na Fedha, Uongozi na Uendeshaji katika Serikali za Mitaa, Maendeleo ya Jamii na Menejimenti ya Rasilimali Watu. Idadi hii ya wanafunzi waliodahiliwa na wale wanaoendelea na masomo inafanya Wanafunzi wote kufikia 2,491 kwa mwaka wa masomo 2013/2014.

Idadi hii ni sawa na ongezeko la asilimia 96.5%  ukilinganisha na jumla  ya wanafunzi 86 waliodahiliwa katika mwaka wa masomo 2007/2008. Kimsingi Idadi ya Wanafunzi wanaojiunga na Chuo hiki imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka kuanzia mwaka wa Masomo 2007/2008, kwa sababu zifuatazo:-
  1. Kuongezeka kwa kozi kutoka kozi nne (4) za awali mpaka kozi nane(8) kwa sasa.
  2. Kuongezeka kwa Watumishi Wanataaluma na Waendeshaji kutoka 38 mwaka 2007/2008 hadi 108 mwaka 2013/2014
  3. Kuongezeka kwa miundombinu mipya ya kujifunzia na kufundishia kama ifuatavyo:-
    1. Mabweni (8) yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 1,620 jumla;
    1. Madarasa (8) yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 jumla;
    2. Ofisi (8) zenye uwezo wa kuchukua zaidi ya watumishi 10;
    3. Maktaba yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 300 kwa pamoja;
    4. Maabara ya kompyuta yenye uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 300 kwa pamoja;
    5. Bwalo la chakula na jiko la kisasa lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 300 kwa pamoja;
    6. Nyumba za makazi ya Watumishi (15), yaani daraja A (5) na daraja B(10);
    7. Ukumbi wa kutolea mihadhara namba 3 ambao una uwezo wa kubeba watu 576;
    8. Kumbi za mihadhara namba moja na namba mbili zenye uwezo wa kubeba watu 400;
Aidha, Chuo kimeanza ujenzi wa Kituo cha Afya cha kisasa kitakachogharimu kiasi cha shilingi bilioni 7.8 Lengo kubwa la ujenzi wa kituo hiki ni kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa Wagonjwa wapatao 3000 wajumuiya ya Chuo ikiwemo wanakijiji waliozunguka Chuo.
Chuo cha Serikali za Mitaa ni miongoni mwa Taasisi zilizoko chini ya OWM-TAMISEMI na kilianzishwa kwa mujibu wa Sheria Na. 26 ya mwaka 1994 (Sura ya 396 toleo lililorejewa mwaka 2002). Lengo kuu la kuanzishwa kwake ni kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kutoa huduma bora zitakazowajengea wananchi uwezo wa kuimarisha utawala bora, kuondokana na umaskini na kuboresha maisha yao.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top