Timu
ya Taifa ya wanawake kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 inawasili
nchini kesho (Ijumaa, Oktoba 25 mwaka huu) saa 8.30 mchana tayari kwa
mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania
itakayofanyika Jumamosi (Oktoba 26 mwaka huu).
Msumbiji
itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege
ya LAM ikiwa na msafara wa watu 25 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi
na viongozi. Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya Sapphire iliyopo maeneo
ya Gerezani, Dar es Salaam.
Mara
baada ya kuwasili JNIA, kocha na nahodha wa timu hiyo watazungumza na
waandishi wa habari juu ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Kwa
upande wa U20 chini ya Kocha Rogasian Kaijage imejiandaa vizuri kwa
ajili ya mechi hiyo, na kesho saa 10 jioni itafanya mazoezi yake ya
mwisho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Viingilio
kwa mechi hiyo ni sh. 1,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na rangi
ya chungwa. Viingilio vingine ni sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP
B wakati VIP A itakuwa sh. 10,000.
Kamishna
wa mechi hiyo Evelyn Awuor kutoka Kenya tayari amewasili nchini wakati
waamuzi kutoka Burundi wanatarajia kuwasili leo saa 1 usiku kwa ndege ya
Kenya Airways wakiunganishia safari yao Nairobi, Kenya. Maofisa wote wa
mechi hiyo wanafikia hoteli ya New Africa.
UCHAGUZI TPL BOARD KUFANYIKA IJUMAA
Uchaguzi
wa Bodi ya Ligi Tanzania (Tanzania Professional League- TPL Board)
unafanyika kesho (Oktoba 25 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano uliopo
Golden Jubilee Tower kuanzia saa 3 asubuhi.
Mgeni
rasmi katika mkutano huo wa Bodi ya TPL ambao unafanyika kwa mara ya
kwanza atakuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Leodegar Tenga.
Kwa
mujibu wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, wajumbe wanaounda Mkutano wa
Uchaguzi ni wenyeviti kutoka klabu 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na
14 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Viongozi
wa klabu za FDL wamefikia hoteli ya Royal Valentino iliyoko Barabara ya
Uhuru wakati wale wa VPL ambao pia watashiriki Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wamefikia hoteli ya Landmark
iliyopo Ubungo.
Wagombea
kwenye uchaguzi huo ni Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti), Said Muhammad
Said Abeid (Makamu Mwenyekiti) wakati wanaoumba ujumbe wa Kamati ya
Uendeshaji ni Khatib Omari Mwindadi na Kazimoto Muzo.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Post a Comment