Ametaka agizo hilo kutekelezwa baada ya wiki mbili kuanzia sasa na kuitaka Mamlaka ya Bandarini (TPA) kumpelekea ripoti kila wiki juu ya utendaji kazi wa vitengo hivyo ikiwamo siku za sikukuu na mwishoni mwa wiki. Dk. Mwakyembe alionya watakaoshindwa kufanya hivyo watafukuzwa na kazi hiyo kupewa watu wengine wanaoweza kazi hiyo.
Waziri huyo ambaye alikuwa amefuatana na Mkuu wa Mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa sasa (Big Result Now) (BRN), Omari Issa, alisema hayo jana wakati alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam kuangalia utendaji kazi wa mamlaka hiyo.
"Vitengo vya bandari vinafanya kazi kama bandari, vinatakiwa vifanye kazi hata siku za sikukuu ili kuendana na kasi kubwa ya ukuaji uchumi, watakaoshindwa tutawafuta na kuwaamuru wateja wasilipie mizigo yao siku vitengo hivyo vinapokuwa havifanyi kazi" alisema Dk. Mwakyembe.
Awali akizungumza katika ziara hiyo, Mtendaji Mkuu wa BRN, Omar Issa alisema bandari ni rasilimali kubwa kuliko rasilimali nyingine kama madini na gesi kwa kuwa vitakwisha lakini bandari itabakia siku zote.
Nae Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Awadhi Massawe alisema bandari hiyo ina mafanikio makubwa kama kuongezeka kwa shehena za mizigo pamoja na magari baada ya kupunguza siku za kutoa mizigo kutoka siku 21 hadi tatu kitu pia kilichopunguza malamiko toka kwa wateja.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment