Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HAYA HAPA MAJINA MAPYA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI


 




Maelekezo Muhimu.

1.Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2013, kidato cha nne mwaka 2012 na JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo, Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea, Mbweni, Maramba, Chita, Makutupola, Mtabila, Msange, Mgulani wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi.
2.Wahitimu hawa waliochaguliwa baada ya usaili wanatakiwa kuripoti tarehe 08/11/2013 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapa chini ili waandaliwe usafiri wa kuwapeleka Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi tarehe 09/11/2013.
3.Zoezi la usajili litaanza chuoni hapo tarehe 10/11/2013 hadi tarehe 15/11/2013.
4.Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi.
5.Vijana hawa watalazimika kufika chuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
a)Vyeti vyao vyote vya masomo( original Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
b)Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)
c)Chandarua chenye upana futi tatu
d)Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)
e)Pasi ya Mkaa
f)Ndoo moja
g)Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingihamsini na mia nne tu (50,400/=).
h)Pesa kidogo ya kujikimu.
6.Kwa mujibu wa kanuni za chuo ni marufuku kufika chuoni na simu ya mkononi. Atakayepatikana na simu atafukuzwa chuoni hapo. Chuo kitaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano.
7.Angalia orodha ifuatayo;
 1.WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2013 NA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top