Vitendo
vya ubakaji vimeendelea kuumiza akili za wapigania haki na ustawi wa
wanawake nchini Tanzania kwa muda mrefu sasa. Miongoni mwa kesi hizi
zimehusisha wasichana wadogo wenye malengo makubwa katika maisha yao,
lakini kutokana na mfumo uliopo, jamii hushindwa kutoa msaada kwa
wahanga wa matukio hayo ili wafanikishe malengo yao.
Emma
Roberts ni binti mwanafunzi aliyekumbwa na mkasa wa kufukuzwa shule
kutokana na ujauzito alioupata baada ya kubakwa. Kupitia kipindi cha
Wanawake Live kinachorushwa na East Africa Television kila Jumanne saa
tatu usiku, binti Emma anaelezea tamaa yake ya kufanya mtihani mwezi
Novemba, kwa kuwa anaamini kuwa elimu itamsaidia yeye na mwanaye ambaye
atalelewa bila kuwa na baba. Kitendo cha kufukuzwa shule kwa tukio kama
hili kumemuathiri kwa kiasi kikubwa, na sasa ana hofu ya kutimia kwa
malengo yake hapo baadae.
Kumnyima
fursa hiyo ya kuendeleza elimu yake ni kutengeneza taifa lenye wanawake
wasio elimu na masikini. Kitendo kilichomkuta Emma, kinaweza kuwakuta
wasichana wengi nchini Tanzania. Kuna wale waliojitokeza hadharani,
lakini vipi kuhusu wale walioamua kukaa kimya?
Joyce Kiria akiwa amembeba mtoto wa Emma. MSIKILIZE KATIKA PICHA HII YA VIDEO BINTI HUYU NA MAMA YAKE.
SOURCE: www.wanawakelivetv.com
Post a Comment