Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HUDUMA YA TRENI YA JIJI DAR ES SALAAM ALMAARUFU TRENI YA MWAKYEMBE YAKWAA KISIKI

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania -TRL  umetangaza kusitishwa kwa huduma ya treni ya jiji hapo leo Jumatatu Oktoba 21, 2013 kufuatia ukarabati wa vichwa cha treni  vinavyotoa huduma hiyo kutokamilika kwa wakati.katika karakana ya Morogoro.

Taarifa za kiufundi zimebainisha kuwa ukarabati wa vichwa hivyo utakamilika mapema leo asubuhi na hivyo kuwasili  Dar jioni tayari kuanza huduma keshokutwa Jumanne, Oktoba 22, 2013 kwa mujibu wa ratiba yake ya kawaida..
Kuhusu kichwa cha treni kilichopata hitilafu ya kuungua moto jana jioni kikiwa safarini kutoka stesheni ya Kamata kuja kituo kikuu cha Dar ni miongoni  mwa ya vichwa vitatu vinavyofanyiwa ukarabati huko Morogoro.
Ukiwaomba radhi Wakazi wa jiji ambao ni watumiaji wakubwa wa huduma hiyo inayoanzia Stesheni ya Ubungo Maziwa hadi Stesheni ya Dar es salaam, Uongozi umewahakikishia kuwa mafundi wa TRL katika karakana za Morogoro na Dar es Salaam wanafanya kila jitihada kurejesha huduma hiyo kwa wakati ili kupunguza usumbufu kwa wateja.wake ambao wameizoeya sana huduma na kunufaika nayo.
Imetolewa kwa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaaam,
Oktoba 20, 2013
 
Midladjy Maez
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top