Ndugu wa marehemu Frank Shoka aliyetuhumiwa kwa wizi wa kuku mwili wake ukisubiriwa kuja kuchukuliwa na polisi |
Hata
hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati polisi wakisubiriwa
mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai moja na kuwaaacha wananchi
katika hali ya mshangao.
|
WAKATI
jeshi la polisi Mkoani Mbeya likijitahidi kutoa elimu kwa wananchi
kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, bado hali imezidi kushamiri
baada watu wawili kuuawa kwa tuhuma za wizi wa mifugo.
Matukio
hayo ywmetokea katika Wilaya za Kyela na Mbeya vijiji yakiwemo ya wizi
wa kuku na ng’ombe jambo lililopelekea wananchi kujichukulia sheria
mkononi kwa kuwaua bila kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.
Katika
Tukio la kwanza lililotokea katika kitongoji cha Katusi kijiji cha
Mjere wilaya ya Mbeya vijijini wananchi wamemuua Frank William Shoka(30)
kwa tuhuma za wizi wa kuku watatu mali ya Dismas Rashid(41)mkazi wa
kijiji hicho.
Akizungumzia
tukio hilo, Dismas Rashidi aliyeibiwa kuku hao alisema tukio hilo
lilitokea Oktoba 20,mwaka huu na kuongeza kuwa marehemu alivunja banda
la kuku majira ya usiku wa manane na kuchukua kuku watatu wakati yeye
akiwa amekwenda kumuuguza mwanae katika kituo cha Afya Mjere ambako
aliandikiwa sindano za masaa.
Alisema
Baada ya kurudi nyumbani na kukuta kuku wake hawapo alianza kufuatilia
na kumkuta marehemu akiwa na kuku hao katika kituo cha mabasi akitaka
kuwasafirisha kwenda Mbeya,alipoulizwa juu ya kuku hao alikosa majibu
wakati huo ikiwa ni saa kumi na moja alfajiri.
Alisema
mtuhumiwa huyo baada ya kushindwa kutolea maelezo juu ya kuku hao
wananchi walianza kumpiga kwa kutumia fimbo na mawe sehemu mbalimbali za
mwili wake hali iliyomfanya kupoteza maisha papo hapo mita chache kabla
ya kufikishwa katika ofisi ya kijiji.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula amesema alipata taarifa za
tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo
alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji hicho Evarist Benny ambaye alitoa
taarifa kituo cha polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi ambapo
Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa
marehemu.
Aidha
Baada mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi na Daktari mwili
ulikabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa taratibu za maziko,hata hivyo
wakati wa tukio hilo mke wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Mary
Julius[30]alikuwa hayupo nyumbani akidai kuwa walikuwa wametengana.
Hata
hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati polisi wakisubiriwa
mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai moja na kuwaaacha wananchi
katika hali ya mshangao.
Katika
tukio la pili lililotokea kijiji cha Lupembe kata ya Katumba Songwe
tarafa ya Unyakyusa wilaya ya Kyela Godfrey Mwakapalila mkazi wa kijiji
cha Mpunguti aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na
kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi.
Chanzo
cha mauaji hayo ni wizi wa ng’ombe mali ya Moto Mwakiange(36) mkulima
na mkazi wa kijiji cha Muungano tukio lililotokea majira ya saa mbili
asubuhi octoba,19 mwaka huu.
Kutokana
na tukio hilo, Jeshi la polisi linamshikilia Moto Mwakiange kwa
mahojiano zaidi wakati upelelezi ukiendelea wa kuwabaini watu
waliohusika na mauaji,aidha mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa
ajili ya taratibu za mazishi.
Kamanda
wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa
matukio yote hayo na kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya
kujichukulia sheria mkoani na atahakikisha wale wote waliohusika na
mauaji wanakamatwa ili kujibu tuhuma za mauaji.
Picha na Ezekia Kamanga
Mbeya yetu
|
Post a Comment