Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
Jeshi
la Polisi Mkoani Singida limefanikiwa kupata mabaki ya mifupa ya mtu
anayedhaniwa kuwa ni Saidi Ngereza (35) mkazi wa Dominiki wilaya ya
Mkalama.
Inadaiwa
Septemba 30 mwaka huu saa 2.30 usiku Saidi alimuaga mke wake Aziza
Khamisi (22) kuwa anakwenda kwa jirani yake kwa ajili ya kumjulia hali
kwa vile alikuwa akiumwa.
Habari
zaidi zinadai kuwa toka siku hiyo aliyoaga hakurudi nyumbani kwake hadi
oktoba 14 mwaka huu saa 6.00 mchana makaki ya mifupa yake
yalipogunduliwa hatua kilomita tatu toka nyumbani kwake.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Geofrey Kamwela amesema mke wa Saidi,
Aziza,aliweza kutambua kuwa mabaki ya mifupa hiyo ni ya mume wake
kutokana na nguo zilizokutwa karibu na mabaki ya mifupa hiyo.
“Aziza
alitambua nguo hizo ambazo ni suruali ya jeans na bukta nyeusi alizovaa
mume wake siku ya Septemba 30 wakati anaaga kwenda kwa jirani kumjulia
hali”,alifafanua Kamwela.
Aidha
amesema baada ya mabaki ya mifupa hiyo kufanyiwa uchunguzi na daktari
ilionekana kuwa marehemu Saidi alipigwa na kitu kizito kichwani na pia
kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
“Uchunguzi
wa awali wa polisi pia unaonyesha kuwa mara baada ya mtu huyo Saidi
kupigwa na kuuawa alifukiwa kwenye shimo lenye kina kifupi Fisi waliweza
kufukua mwili huo kutokana na harufu kali na kuula na kubakisha
mifupa”,amesema Kamwela.
Kamanda
Kamwela amesema kwa sasa wanawashikilia watu wawili kwa mahojiano
kuhusiana na mauaji hayo Kwa sasa hatuwezi kutaja majina ya watu
tunaowashikilia kwa sababu kitendo hicho kinaweza kuvuruga upelelezi.
Hata
hivyo amesema mtuhumiwa mmoja ambaye Saidi (marehemu) aliaga kuwa
anaenda kwake kumjulia hali baskeli ya marehemu aliyoondoka nayo
ilikutwa kwake.



Post a Comment