
Eneo la tukio Washington DC ambapo Omar Sykes (picha ya ndani) aliuawa.
Photo Credits: National Review Online
Jumanne
wiki hii, idara ya Polisi Washington DC (Metropolitan Police
Department) ilitangaza kukamatwa kwa mtuhumiwa mmoja kati ya wawili
waliokuwa wakitafutwa kwa mauaji ya mwanafunzi mTanzania aliyekuwa
akisoma katika chuo kikuu cha Howard hapa jijini.
Omar Sykes (22) aliuawa usiku wa Julai 4 mwaka huu nje kidogo ya maeneo ya chuo hicho alipokuwa pamoja na mwenzake.
Wakiwa
mtaa mmoja toka chuoni, wanafunzi hao walivamiwa na watu wenye silaha
waliotaka kuwapora, na katika harakati hizo, Omar alipigwa risasi
kifuani na kufariki.
Hii ni
sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA
DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam
Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es
Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Oktoba 19, 2013


Post a Comment