Baadhi
ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Morogoro wakiwakilisha Vyombo
mbalimbali vya Habari hapa nchini wakifanya mahojiano mafupi na Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) mara baada ya
kufunga rasmi Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza
katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza waliosimama
katika picha mara baada ya kufunga rasmi Mkutano Mkuu wa Maafisa
Waandamizi wa Magereza Oktoba 25, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema,
Mkoani Morogoro(wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Haji Janabi(wa pili kulia) ni
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Alhaj Jumanne Mangara(wa tatu kulia)
ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa
tatu kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga. Wengine ni
Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James
Selestine na Mkuu wa Magereza Mkoani Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza,
Editha Mallya. Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba ya
ufungaji wa Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza
uliomalizika leo Oktoba 25, katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani
Morogoro.
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati
akitoa hotuba ya ufungaji wa Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi
la Magereza uliomalizika leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani
Morogoro.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa pili kulia) akitolea
ufafanuzi baadhi ya hoja mbalimbali zilizojitokeza katika Mkutano Mkuu
wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kabla ya kufunga rasmi
Mkutano huo leo Oktoba 25, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani
Morogoro.
Post a Comment