Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CHINA KUTOA MSAADA WA DOLA MILIONI SITA KWA ZANZIBAR

 


903aOmar-Yussuf-MzeeNa Ali Issa na Mariam Fumu Maelezo-Zanzibar
……………………………………………….
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana Saini mkataba wa
makubaliano na Serikali ya China  ambapo nchi hiyo itaipatia Zanzibar
msaada wa zaidi ya  Dola milioni sita za Marekani ikiwa ni uendelezaji
wa misaada inayotolewa na nchi hiyo kwa Zanzibar katika nyanja mbali
mbali za Uchumi.
Sherehe za utiaji saini makubaliano hayo  zilifanyika leo  katika
Wizara ya Fedha, Vuga  ambapo Waziri wa Wizara hiyo  Omar Yussuf Mzee
aliiwakilisha Zanzibar na Balozi mdogo wa China hapa Zanzibar Xie
Yunliang aliiwakilisha nchi yake.

Akizungumza baada ya utiaji saini, Waziri wa Fedha alisema kua msaada
huo utalenga katika nyanja mbali mbali ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya
Abdalla Mzee Mkoani, Uchimbaji wa visima vya maji safi na salama na
kupambana na mbu wa malaria  katika maeneo ambayo maradhi hayo bado
yapo.


Alisema kazi iliobakia hivi sasa ni kwa Idara ya   Hazina kuwasiliana
na wahusika  ili utekelezaji wa makusudio hayo yaweze kufikiwa kwa
haraka.

Nae Balozi Xie Yunliang alisema kuwa  Zanzibar na China ni nchi mbili
zenye uhusiano mzuri  wa muda mrefu hali ambayo imeifanya kua ni
rafiki wa karibu.

Alisema  makubaliano hayo ni muendelezo wa misaada wanayoitowa ili
kuona Zanzibar inapiga hatua katika juhudi zake za kukuza Uchumi na
Maendeleo ya wananchi.

Utiaji saini makubaliano hayo ulikwenda  sambamba na  kukabidhiwa hati
za Taa za Barabarani zinazo tumia nishati ya jua katika Manispaa ya
Mji wa Zanzibar ambapo mradi huo ulifadhiliwa na Serikali ya China.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top