WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda ameawaonya baadhi ya Watanzania wengi wanaokuja
katika jiji la Guangzhou nchini China kwa ajili ya kununua bidhaa
mbalimbali waache kuuza hati zao za kusafiria kwa raia wa nchi nyingine
kama njia ya kujiongeza kipato.
Ametoa onyo hilo jana usiku (Alhamisi, Oktoba 24, 2013) wakati akizungumza Watanzania
wanaofanya biashara na wale wanaoishi katika jiji la Guangzhou, jimbo
la Guangdong ambalo ni jiji kubwa la biashara lililoko kusini mwa China.
Alisema
kuwa wengi wa wafanyabiashara hao wanapouza pasipoti zao wanasingizia
kuwa zimepotea ndio maana kuna malalamiko mengi kutoka kwa Watanzania
wanaofika katika jimbo hilo kudai wanaibiwa hati zao za kusafiria wakati
sio kweli.
Wakati
wa mazungumzo hayo, mmoja wa Watanzania hao aliyejitambulisha kwa jina
la Ambrose Lugai alisema changamoto nyingi zinazowakabili Watanzania
waishio katika jimbo hilo na moja ya tatizo hilo ni kuibiwa kwa hati za
kusafiria za Watanzania.
Bw.
Lugai alisema tatizo la wafanyabiashara wengi kupoteza pasipoti
limekuwa sugu na kila siku linaongezeka na cha ajabu linawatokea
wafanyabiashara wa kutoka Tanzania tu.
“Hatuwezi
kusema ni u-carelessnes, lakini jamii ya hapa ni kutoka mataifa
mbalimbali, inakuwaje pasipoti za Tanzania tu ndio zinakuwa hot cake,
naomba utusaidie namna ya kulinda hati hizi,” alisema Bw. Lugai.
Alimwomba
Waziri Mkuu awasaidie kuzungumza na Serikali ya jimbo hilo ili
Watanzania wawe wanaacha pasipoti hotelini wakati wanapoenda mitaani,
badala yake wapewe karatasi nyingine ya kuwatambulisha huko mitaani.
Katika
kujibu hoja hiyo ya Bw. Lugai, Waziri Mkuu alisema kwamba suala hilo
linamshangaza kwamba inakuwaje hati za wafanyabiashara wa Tanzania tu
ndio zinaiibiwa wakati wafanyabiashara wanaofika kwenye jimbo hilo ni
wengi kutoka mataifa mbalimbali. “Kupoteza
pasipoti ni jambo la nadra sana, sio la kawaida. Nilitegemea hili
linaweza kumtokea mtu mmoja mmoja, lakini nashangazwa kwamba hapa
Goangzhou ni tatizo kubwa.”
“Lakini
taarifa nilizo nazo nyie wenyewe wafanyabiashara mnauza hati zenu kwa
Wanaigeria ili mpate fedha za kufanyia biashara. Ndio maana nawasihi
achani haya mambo, mnajifedhehesha wenyewe na mnaifedhehesha nchi,”
alisema Waziri Mkuu.
Alisema
kwa kuwa tatizo hilo ni kubwa na akamtaka balozi wa Tanzania nchini
China, Luteni Jenerali mstaafu Abdulrahman Shimbo afuatilie kwa karibu
kujua idadi ya watu walioibiwa hati zao za kusafiria ili Serikali iweze
kulishughulikia.
“Lakini
nawaonya acheni tabia mbaya ya kuuza pasipoti zenu kwa tamaa ya kupata
vijipesa vidogo vidogo hivyo, hii ni kuivunjia nchi heshima,” alisema.
Lakini
pia alitaka jumuiya ya Watanzania waishio China kuimarishwa zaidi ili
wawe na uwezo wa kushughulikia kero zao mbalimbali zinazowakabili wakiwa
katika ugenini. Alisema ni kuimarika kwa jumuiya hiyo tu kutawasaidia
wanafunzi na wafanyabiashara kufikisha malalamiko yao haraka
serikalini.
Post a Comment