Mkurugenzi
wa Fedha wa Bohari ya Dawa (MSD), Joseph Tesha (wa pili kushoto),
akimkabidhi msaada wa fulana Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT),
Dk.Primus Saidia Dar es Salaam juzi, kwaajili ya mkutano mkuu wa mwaka
wa MAT utakaofanyika Novemba 28 na 29 katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili.Wengine katika picha kulia ni Meneja wa Huduma kwa Wateja na
Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia na Ofisa Misaada wa MSD, Milton
Kigwinya. (PICHA NA DOTTO MWAIBALE)
………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD), imetoa msaada wa fulana 300 zenye thamani ya sh.5.5milioni kwa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), kwa ajili ya mkutano mkuu wa chama hicho utakaofanyika Novemba 28 na 29 mwaka huu.
Akizungumza katika hafla ya utoaji
wa msaada huo iliyofanyika juzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
Fedha wa MSD, Joseph Tesha alisema wanajisikia fahari kushirikiana na
madaktari hao kwani wao ni kitu kimoja.
“Kuwa jirani na chama hicho cha
madaktari ni fursa pekee ya kupata maoni na ushauri wa kiutendaji baina
ya makundi hayo mawili” alisema Tesha.
Alisema MSD inatoa huduma kwa
wananchi moja kwa moja hivyo kupitia madaktari hao wanaweza kupata maoni
yao ambayo yatafanyiwakazi na kusaidia maendeleo katika sekta hiyo
muhimu kwa taifa la Tanzania.
Aliongeza kuwa MSD itashiriki
katika maonyesho yaliyoandaliwa na MAT wakati wa siku za mkutano huo kwa
kuonesha vifaa tiba vipya pamoja na kuzungumza na wadau wake wakuu wa
afya ambao ni madaktari.
Katika hatua nyingine MSD
inatarajia kuzindua mpango mkakati wa mwaka 2014 – 2020, ambapo pamoja
na mambo mengine unazungumzia uboreshaji wa usambazaji dawa na vifaa
tiba.
Kwa upande wake Rais wa Chama cha
Madaktari Tanzania (MAT) Dk. Primus Saidia alisema chama chenye
wanachama wapatao 1358 kimekuwa kikilishiriana na makundi mengine katika
sekta ya afya.
Alisema kwa upande wao ni fursa
nyingine ya kipekee kushirikiana na MSD ili kuwaeleza yale
wanayokabiliana nayo katika utendaji wao wa kila siku hasa katika
masuala ya dawa na vifaa tiba.
Dk. Saidia alitumia fursa hiyo
kuishukuru MSD kwa msaada huo ambao umetolewa katika kipindi muafaka cha
mkutano mkuu wa chama hicho.
Post a Comment