Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, JOHN CASMIR MINJA AMVISHA CHEO CHA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA MAGEREZA ALIYEKUWA ANASHIRIKI ULINZI WA AMANI KATIKA JIMBO LA DARFUR - SUDAN, LEO JIJINI DAR


Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) akimvisha
Cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Kato
Rugainunura ambaye anahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la
Darful - Sudan. Hafla ya uvalishaji cheo imefanyika leo Oktoba 30, 2013
katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini
Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja( kulia)
akimpongeza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Kato
Rugainunura mara baada ya kumvisha cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la  Magereza, Jijini Dar es Salaam. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa  Magereza, Dkt. Kato Rugainunura ni miongoni mwa Maafisa wa Jeshi la  Magereza ambao wanahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darful - Sudan.
 Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini walioshiriki
hafla fupi ya uvishaji cheo kwa Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Magereza
ambaye amevishwa cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza na  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani).
 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa nasaha
fupi mara baada ya zoezi la uvalishaji cheo kwa Kamishna Msaidizi  Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Kato Rugainunura( hayupo pichani) ambaye  kwa sasa anahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darful - Sudan.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Kato
Rugainunura(aliyesimama) akitoa neno la shukrani kwa Kamishna Jenerali
wa Magereza nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani) mara baada ya
zoezi la uvalishaji cheo lililofanyika leo Oktoba 30, 2013 katika Ukumbi
wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam(
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top