Mamia
ya wakazi wa Kibaha mkoani pwani pamoja na jiji la Dar es Salaam leo
walimiminika kwa wingi nyumbani kwa Marehemu Anastazia Saro Kibamba
Kibwegere kutoa heshima za mwisho kwa mama wa Mwanahabari Ufoo Saro
aliye uwawa kwa kupigwa risasi na mzazi mwenza wa binti yake huyo ambaye
pia alijeruhiwa kwa risasi.
Kwa mujibu wa ripoti ya madkatari
walioufanyia uvchunguzi mwili wa Marehemu, Muuaji ambaye alitambulika
kwa jina la Anthery Mushi ambaye nae alijiua baada ya kutekeleza tukio
hilo alimpiga risasi tano.
Mwili wa marehemu ukiingizwa katika
Kanisa la KKKT Mtaa wa Kibwegere Kibamba kwa misa maalum,. Marehemu
alikuwa akiimba kwaya ya Usharika huo.
Mwili wa marehemu ukiwa nyumbani kwake.
Mwili ukiwa ndani Kanisani
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho wakiongozwa na baba mchungaji
Mkurugenzi wa ITV na Redio One, Joyce Mhavile akitoa heshima za mwishi. Picha ya juu ni mwana jamii.
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho pamoja na wanakwaya wenzake na Marehemu.
Mtoto wa Ufoo, Alvin Mushi akiwa na
masikitiko na majonzi makubwa baada ya kuondokewa na Bibi yake. Alvin
anadaiwa kulelewa na Bibi na Babu.
Waombolezaji wakiwa kanisani hapo.
Wapili kulia ni Mkurugenzi wa ITV na Redio One, Joyce Mhavile ambaye
wakati wa salamu zake alidai amemwakilisha Ufoo Saro ambaye yupo
Hospitali na ameshindwa kuja kumuaga mama yake. Na amefanya hivyo
kutokana na ombi la Ufoo.
Waombolezaji...
Rafiki wa siku nyingi wa Ufoo Saro,
Julieth Ngalabali kutoka gazeti la Mwananchi akiwa amebebna shada la
maua na mwombolezaji mwingine.
Wanahabari waliofika msibani hapo.
Nje ya Kanisa hilo.Picha Zote na Mdau Mroki Mroki
----
Mtaalam aeleza kwa nini muuaji aliua
Anazikwa leo kijijini Shari,Machame
Mtaalam aeleza kwa nini muuaji aliua
Anazikwa leo kijijini Shari,Machame
Mwili
wa Anastazia Saro, mama mzazi wa mtangazaji na mwandishi wa kituo cha
Televisheni cha ITV, Ufoo Saro, aliyeuawa kwa kupigwa risasi Jumapili
iliyopita, ulifanyiwa uchunguzi jana kwenye Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH), na kukutwa na risasi tano.
Anastazia aliyeuawa wakati akisuluhisha ugomvi kati ya binti yake Ufoo
na mzazi mwenzie, Anthery Mushi, alikutwa na risasi hizo katika sehemu
kadhaa za mwili wake.
Mushi mbali na kumuua Anastazia, pia alimjeruhi kwa risasi Ufoo kisha kujilipua mwenyewe na kufariki dunia papo hapo.
Hayo
yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Allelio Swai, Mwenyekiti wa
kamati ya mazishi ya Anastazia wakati akizungumza na NIPASHE muda mfupi
kabla ya mwili huo kutolewa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha
hospitali hiyo, na kupelekwa Kibamba kwa ajili ya ibada ya mazishi
tayari kusafirishwa kwenda Machame kijiji cha Shari kwa ajili ya mazishi
leo.
Swai
alisema kuwa katika uchunguzi wa mwili huo ambao hata hivyo, hakumtaja
daktari aliyeufanya, baadhi ya ndugu wa marehemu walihudhuria.
Swai alifafanua kuwa risasi hizo zilikutwa katika maeneo ya mapafu, maini na tumbo.
Kwa
mujibu wa Swai mwili huo ulitakiwa kufanyiwa uchunguzi mapema asubuhi,
lakini ulichelewa kutokana daktari huyo kuwa na majukunu mengine,
walilazimika kusubiri kwa muda.
Mwili wa mama huyo uliondolewa hospitalini hapo saa 7:30 mchana baada ya kukamilika kwa taratibu zote.
Daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili huo na kuondoa risasi hizo,
alikataa kuzungumza chochote zaidi ya kusema: “Siwezi kulizungumzia
jambo hili kwa kuwa nimeshakamilisha nilichotakiwa kukifanya.”
Baadhi ya ndugu wa marehemu Anastazia waliokuwapo eneo hilo na
walioshuhudia uchunguzi wa mwili, walisikika wakisema kuwa kitendo
alichokifanya Mushi ni cha kinyama kutokana na kutumia risasi nyingi
kumuua ndugu yao.
Wakati huo huo, Ufoo hataweza kushiriki mazishi ya mama yake kutokana na matibabu anayoendelea kuyapata, hospitalini hapo.
Swai
aliiambia NIPASHE kuwa walimtaarifu Ufoo juu ya mipango ya mazishi ya
mama yake na kwamba naye ametoa ruhusa ili mama huyo azikwe hata kama
yeye (Saro) hataweza kuhudhuria mazishi hayo kutokana na hali yake.
“Niliongea na Ufoo ili kumfahamisha kuhusu mipango ya mazishi naye
alitutaka tuendelee na mipango hiyo hata kama yeye atashindwa kumzika
mama yake, lakini cha msingi alituomba tuhakikishe kuwa mama yake
anazikwa salama,” alisema Swai.
MWANASAIKOLOJIA AMZUNGUMZIA MUSHI Wakati hayo yakijiri, Mhadhiri Mwandamizi katika mambo ya Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Kitila Mkumbo, amesema kulingana na taarifa za mauaji ambazo amekuwa akizisoma kwenye vyombo vya habari juu ya mauaji hayo yalivyofanyika, ni dhahiri muuaji alikuwa amefikia ngazi ambayo hasingeweza kuacha kufanya unyama huo.
MWANASAIKOLOJIA AMZUNGUMZIA MUSHI Wakati hayo yakijiri, Mhadhiri Mwandamizi katika mambo ya Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Kitila Mkumbo, amesema kulingana na taarifa za mauaji ambazo amekuwa akizisoma kwenye vyombo vya habari juu ya mauaji hayo yalivyofanyika, ni dhahiri muuaji alikuwa amefikia ngazi ambayo hasingeweza kuacha kufanya unyama huo.
Alisema mtu huyo alikuwa amejiandaa kufanya tukio hilo kwa muda mrefu kimkakati na kimaandalizi.
Alifafanua kuwa mhusika wa tukio hilo alikuwa ameshafikia katika hatua
ya mwisho ya maamuzi inayoitwa tafsiri ya akili ambayo huwa ni vigumu
kwa mtu kujizuia kutenda jambo.
Alisema kuna hatua tatu ambazo ni stress (msongo wa mawazo), depression
(sonona) na tafsiri ya akili ambazo mtu anaweza kuzipitia kabla
hajachukua maamuzi.
“Kuna kitu kinaitwa fluctuation, lazima kilitokea kati yake na familia
hiyo siyo bure, lakini angekuwapo yeye mwenyewe angetueleza, sisi
hatuwezi kujua,” alisema Dk. Mkumbo.
Dk.
Mkumbo alisema kuwa sehemu aliyokuwa anafanya kazi marehemu Mushi
(Darfur) siyo kigezo kikubwa cha kuamua kufanya tukio lile japokuwa watu
wengi wanaoishi katika mazingira ya kuona maiti za watu huwa ni wepesi
kuua.
Alisema hicho siyo kigezo cha marehemu kufanya kitendo hicho kwa kuwa hakuna mwanadamu asiyeogopa kifo.
Kuhusiana na iwapo wanajeshi wanaotoka katika operesheni za kijeshi nje
ya nchi kama wanapatiwa ushauri (councelling), Msemaji wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Erick Komba alisema:
“Mafunzo anayopata mwanajeshi yanalenga kumjenga na kumpa uwezo wa
kuyakabili mazingira mbalimbali ndani na nje ya nchi kimaumbile na
kisaikolojia,” alisema.
Meja Komba alisema mwanajeshi ana uwezo wa kuishi kwenye mazingira yoyote kwa kipindi kirefu kijasiri.
“stress management-(jinsi ya kubaliana na msongo) inafanyika vizuri kwa
kufanya michezo mbalimbali kwa pamoja ambayo inaimarisha fiziki
(ukakamavu),”
Aliongeza kuwa maisha ya mwanajeshi ni ya umoja na ushirikiano, kitu
ambacho kinamfanya ayakabili mazingira yake vizuri, na kuweza kutekeleza
majukumu ya jeshi kiufasaha na kiuweledi.
Alisema kwa kipindi wanapokuwa katika operesheni mbalimbali za ulinzi wa amani pamoja na mambo mengine wanapewa ushauri.
HALI YA UFOO YAZIDI KUIMARIKA
Ofisa Habari wa MNH, Aminiel Aligaesha, alisema jana kuwa hali ya Ufoo inaendelea vizuri kulinganisha na siku za nyuma.
Alisema kwa sasa yupo katika jengo la matibabu ya moyo na kueleza kuwa
kwa mujibu wa taarifa ya daktari anayemuhudumia, Ufoo anahitaji
mapumziko zaidi.
“Kwa
sasa Ufoo haitaji kuonana na mtu, anahitaji kupumzika zaidi kama
daktari alivyoniambia na kwa kifupi yupo katika wodi ya kawaida tu,”
alisema Aligaesha.
SIMANZI YATAWALA KUAGA ANASTAZIA
Mwili wa marehemu Anastazia
uliagwa jana katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT)
Usharika wa Kibwegele Kibamba Shule kabla ya kuelekea kijiji cha Shari
Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi.
Waumini na wanakwaya ya Uinjilisti wa Kanisa hilo waliangua vilio baada
ya jeneza la mwili wa marehemu ambaye alikuwa mwanakwaya na mweka hazina
wa kanisa kufika kanisani hapo.
Kadhalika, ibada iligubikwa machozi na simanzi, hali iliyosababisha kusimama kwa muda.
Mchungaji wa Kanisa hilo, Magret Shekolowa, aliwaeleza waumini hao kuwa
na moyo wa subira hasa katika kipindi hiki na kuwataka kuacha kulia
badala yake waiombee Tanzania kwani kumekuwa na matukio mengi ya mauaji
ya kinyama.
Akitoa salamu za rambirambi Mkurugenzi wa ITV, Joyce Mhavile, huku
akitokwa na machozi ya huzuni alisema: “Jana nilikwenda kumuona Ufoo
akaniomba nitoe salama za mwisho nisimame kwa niaba yake, nami nasema
poleni sana.”
Marehemu alizaliwa mwaka 1957 huko Mbulu mkoani Arusha na alifariki juzi baada ya kushambuliwa kwa risasi tano na Mushi.
Imeandikwa na Samson Fridolin, Gwamaka Alipipi, Raphael Kibiriti na Margaret Malisa.
CHANZO: NIPASH
Post a Comment