“PRESS RELEASE” TAREHE 16. 10. 2013.
WILAYA YA CHUNYA – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA SAA 23:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
NKUHUNG’U KATA YA LUPA, TARAFA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA MKOA WA
MBEYA. MATHA D/O CHARLES, MIAKA 32, MFIPA, MKULIMA, MKAZI WA
NKUHUNG’U, ALIFARIKI DUNIA AKIWA NYUMBANI KWAKE BAADA YA KUPIGWA KWA
FIMBO MGONGONI NA MBAVUNI NA MUME WAKE AITWAE JOSEPH S/O JOHN, MIAKA 40,
MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA NKUHUNG’U SIKU YA TAREHE 28.09.2013 MAJIRA
YA SAA 02:45HRS . CHANZO NI UGOMVI WA KIFAMILIA. BAADA YA TUKIO
MTUHUMIWA ALIMKATAZA MAREHEMU KWENDA HOSPITALI KUPATA MATIBABU HIVYO
KUUGULIA NYUMBANI HADI ALIPOFARIKI DUNIA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA
UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA
TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA
WITO KWA JAMII HASA WANAFAMILIA/NDOA KUTATUA MATATIZO YAO KWA KUJENGA
HOJA NA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA
KUEPUKIKA.
WILAYA YA KYELA – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MNAMO
TAREHE 15.10.2013 MAJIRA YA SAA 17:30HRS HUKO KASUMULU WILAYA YA KYELA
MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1. ZALAKA S/O
KABHAM, MIAKA 20 NA 2. ERISIDO S/O KAPARA, MIAKA 25, WOTE RAIA NA WAKAZI
WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU NI
KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO NA KUHIFADHIWA NA DENIS S/O ANORD, MIAKA
20, KYUSA, MKULIMA MKAZI WA KASUMULU AMBAYE PIA AMEKAMATWA. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA
WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA
MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI ILI HATUA
ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE MARA MOJA.
|
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
Post a Comment