Mangula alitoa kauli hiyo jana wakati akiwasilisha mada yake kwenye semina ya watendaji wa Chama hicho iliyomalizika jana mjini Dodoma.
Alisema yuko tayari kuwashukia wakati wowote wale ambao watakuwa wakituhumiwa na kuthibitika kutenda kinyume na chama hicho.
“Pamoja na hayo, hatutakuwa na huruma na viongozi na watendaji wa mikoa wa chama watakaobainika kuwasaidia wagombea wasio waadilifu kupita katika kura za maoni,” alisema Mangula.
Mafunzo hayo maalumu ya siku nne yalifungwa jana jioni na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.
Jumla ya mada 12 katika semina hiyo iliyowahusisha makatibu wa wilaya na mikoa pamoja na wenyeviti wa wilaya ziliwasilishwa.
Kauli hiyo ya Mangula inafuatia watendaji wa chama hicho kulalamikiwa na wanachama wake kuhusiana na utendaji mbovu.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment